Maadhimisho ya siku ya kupambana na Fistula Duniani
yamefanyika huku jamii ikitakiwa kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha
wanawake wenye tatizo hili wanasaidiwa katika kupatiwa matibabu.
Meneja Mradi wa Fistula
katika hospitali ya CCBRT iliyoko Jijini Dar es salaam Clement Ndahani amesema
ni jukumu la kila mmoja katika kumsaidia mwanamke mwenye tatizo hili katika
kuhakikisha anapatiwa matibabu.
Clement amesema jamii inapopata taarifa za mwanamke
mwenye tatizo la fistula ambalo hutokea wakati wa mama huyo huyo akijifungua
kutokana na uzazi pingamizi ni vyema kumpa ushauri katika kuwahi matibabu ili
kumaliza tatizo hilo.
Amesema mpaka sasa matibabu ya Fistula yanatolewa bure
katika hospitali ya CCBRT iliyoko Dar es salaamu lakini katika maeneo mbali
mbali kuna mabalozi wao wakiwemo Redio Fadeco ambapo wanahakikisha mgonjwa
amefika hospitali na kupatiwa matibabu ya tatizo hilo bila malipo yoyote.
Ndahani ametaja dalili kubwa za ugonjwa wa fistula kwa
mwanamke kuwa ni kutokwa mkojo mara kwa mara bila kujizuia na kinyesi kupitia
sehemu ya ukeni hali ambayo siyo ya kawaida kabla ya kupata tatizo hilo.
.
Hata hivyo kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya kupambana
na Fistula mwaka huu ni Tokomeza Fistula sasa ambayo ina lengo la kuhakikisha
jamii inashirikiana kwa pamoja na wanawake wenye tatizo hilo katika
kulitokomeza.
Post a Comment