Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: ULEVI WASABABISHA KIFO CHA MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 2 HUKO WILAYANI MULEBA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Daud mwenye umri wa miaka 21 anayesadikiwa kuwa alikuwa amelewa amesababisha kifo cha Mtoto...

Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Daud mwenye umri wa miaka 21 anayesadikiwa kuwa alikuwa amelewa amesababisha kifo cha Mtoto Sabin Samson mwenye umri wa miaka 2 katika kata ya Burungura Wilayani Muleba baada ya kumgonga na kitu kizito kichwani.

Salome Sabini mama mzazi wa Sabini ameeleza kuwa Mei 22 majira ya saa 12 jioni akiwa amekaa nyumbani kwake na watoto wake wanne alitokea kijana huyo na kuanza kufanya fujo huku akionekana alikuwa amelewa.

Salome ameeleza kuwa baada ya kijana huyo kuanza kufanya fujo katika maeneo hayo ilimbidi aanze kuwakimbiza watoto wake kuwasogeza mbali lakini kutokana na kuwa watoto hao walikuwa wanne na wote ni wadogo ndipo akakuta kijana huyo ameshampiga kichwani mtoto huyo na kitu kizito kichwani.

Amesema katika harakati za kuwahamisha watoto hao alikuta Samsoni anatokwa damu kichwani na kusema kuwa ilibidi naye amuweke pemben na kuanza kutafuta msaada wa majirani na majirani walipofika ndipo wakakuta mtoto huyo tayari amepoteza maisha.

Shuhuda wa tukio hilo ambao ni majirani wa familia hiyo wamesema kijana huyo amekuwa akijihusisha na unywaji wa pombe kali kupita kiasi hali ambayo imekuwa ikimfanya kijana huyo kufanya fujo katika maeneo mbali mbali ambayo yanamzunguka.

Jeshi la Polisi Wilayani Muleba wamefika katika eneo la tukio kisha kuruhusu mwili wa marehemu kuzikwa huku kijana huyo aliyefanya kitendo hicho kushikiliwa na polisi  na wamewataka vijana na jamii kwa ujumla kutojiingiza katika ulevi na badala yake wajikite katika shughuli za uzalishaji.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top