Takwimu za hivi karibuni
hapa nchini zinaonyesha kwamba kwa mwaka, Tanzania inapoteza kina mama 7,900
kutokana na sababu zitokanazo na ujauzito ambapo Idadi hiyo ni sawa na vifo 22
kwa siku.
Magonjwa yanayoongoza
kusababisha vifo vya wazazi nchini na mataifa mengine ni kifafa cha mimba,
uzazi pingamizi, kupoteza damu nyingi wakati na baada ya kujifungua na
maambukizi baada ya kujifungua.
Ofisa Mawasiliano wa
Muungano wa Utepe Mweupe kwa Uzazi Salama, Lydia Kamwaga amesema taarifa nyingi
zimeonyesha bado vituo vingi vya afya havitoi huduma za uzazi za dharura
kutokana na ukosefu wa vifaa kama vile vya upasuaji.
Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia,
wazee na watoto Ummy Mwalimu, ameipongeza zahanati ya Uturo wilayani Mbarali
Mkoani Mbeya kwa kuwa imekuwa mfano wa kuigwa Nchini Tanzania kwa kuzuia vifo
vitokanavyo na mama wajawazito na watoto wachanga.
Aidha, amesema anautambua mchango mkubwa
kwa watoa huduma ngazi ya jamii na kwamba Moja ya kipaumbele chake katika
wizara hii ni kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika.
Kwa upande wao baadhi ya wakinamama ndani
ya wilaya ya kyela wameeleza sababu zinazotokana na vifo kwa wanawake na watoto
pindi walipohojiwa na kituo hiki juu ya sababu zinazosababisha vifo hivyo
kushamiri hapa nchini.
Hata hivyo ili kupunguza vifo hivyo
inashauriwa kuweka mikakati ya kuzuia akina mama kujifungulia nyumbani na kila
mwanaume na mwenza wake kuhakikisha wanahudhuria kliniki kuanzia ujauzito hadi
mtoto anapofikisha umri wa miaka mitano.
Post a Comment