Wananchi wa kijiji cha Katembe kata ya Kituntu wilayani
Karagwe mkoani Kagera wametakiwa kuendelea kuchangia utengenezaji wa madawati
ili kukalimisha zoezi hilo kwa muda unaotakiwa.
Wito huo umetolewa leo na mwenyekiti wa serikali ya
kijiji cha Katembe Innosent Muganyiz.
Muganyizi amesema kuwa tayari wameshahitisha vikao mbalimbali
kwa ajili ya kujadili juu ya uchangiaji wa madawati na tayari wamebainisha
wadau wa maendeleo watakaosaidia katika uchangiaji wa madawati kwa kushirikiana
na wananchi.
Ameongeza kuwa katika mchakato huu wa kuchangisha
madawati wanakumbana na changamoto ikiwemo ya baadhi ya wananchi na viongozi
kuchanganya siasa na maendeleo.
Muganyizi amesema kuwa wananchi wanatakiwa kutambua kuwa
serikali ina nia nzuri katika suala zima la kutoa elimu kwa kila mtanzania .
Post a Comment