Analipwa
kubikiri watoto ili kuondoa mikosi Malawi
Katika
tamaduni nyingi kote duniani mwanamke anapoolewa huwa ni fahari kubwa sana
akiwa ni bikira.
Mathalan
ni dhihirisho la mwanamke kuwa amelelewa na kutunzwa vyema. Ni dhihirisho la
usafi.
Hata
hivyo jamii moja nchini Malawi haithamini ubikira wa watoto wao wa kike.
Amini
usiamini wazazi huwa wanamlipa ''Fisi'' kumbikiri binti yao punde tu anapopata
hedhi yake ya kwanza.
Wanaamini
kuwa binti ambaye ni bikira ni mkosi kwa jamii! Malimwengu haya.
Wazazi
na jamii kwa jumla katika maeneo mengi ya kusini mwa Malawi wamekuwa
wakishikilia tamaduni hii kwa miaka na mikaka.
''Fisi''
ama wanaume wanaowabikiri watoto wa kike huchaguliwa na wazazi kuwaondolea
mikosi.
Na
huwa ni sherehe kubwa inayomtangulia binti kupelekwa unyagoni kisha
kuwatembelea shangazi wake kabla ya kujulishwa kwa fisi.
Amini
usiamini hao mafisi hulipwa takriban dola $7 kwa kila kitendo cha ngono na hao
mabinti ambao wengi huwa na kati ya umri wa miaka 11-14.
Fisi
mmoja katika kijiji cha Nsanje, Eric Aniva ameiambia BBC kuwa hajui kwa kweli
amewabikiri wasichana wangapi, kwa sababu ni wengi.
''Kwa
kweli mimi nimewabikiri zaidi ya wasichana 104," amesema. ''Hii ndiyo
tamaduni yetu''.
''Hapa
mwanamke akifiwa lazima aje kwangu nimuondolee mkosi hata kabla ya kuzikwa kwa
mumewe''.
''Mwanamke
akiavya mimba pia kabla hajarejelea maisha yake ya kawaida ama hata kushiriki
ngono na mwanamume mwengine lazima aje kwangu nimsafishe," alisema fisi
huyo.
Anasema
kuwa pale anaposhiriki ngono na watoto hao huwa anapewa muda wa siku 3 hivi
kumsafisha na kumuondolea mkosi.
Kulingana
na tamaduni zao, ikiwa mwanamke ama binti anakataa asibikiriwe huwa wanaamini
kuwa jamaa zao watafuatwa na mikosi na magonjwa.
Source:
bbc
Post a Comment