Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: MAFANIKIO KIMAISHA HAYAKAI KWENYE VYETI:-
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
MAFANIKIO KIMAISHA HAYAKAI KWENYE VYETI:- Na Albert Nyaluke Sanga Nikiwa mwaka wa kwanza Chuo Kikuu Cha Tumaini- Iringa (sasa wana...

MAFANIKIO KIMAISHA HAYAKAI KWENYE VYETI:-
Na Albert Nyaluke Sanga

Nikiwa mwaka wa kwanza Chuo Kikuu Cha Tumaini- Iringa (sasa wanakiita University Of Iringa); nilikutana na jamaa mmoja aliyekuwa ndio kwanza ametua nchini baada ya kumaliza shahada yake ya kwanza katika moja ya vyuo vikuu nchi ya jirani hapo kwa Museveni.

Jamaa huyu akaniambia kauli ya ajabu sana, akasema, "Kwa nini umeenda kusoma chuo hicho?(akimaanisha Tumaini). Wenye akili wako UDSM(Akimaanisha chuo kikuu cha Dar es Salaam, maarufu kama Mlimani), huko Tumaini umeingia choo cha kike, utachelewa sana kuajiriwa".  Nikamwangalia weeee, (nikamuhurumia na kumdharau ndani kwa ndani) halafu nikamjibu kwa hasira; "Brother, wenye akili ni wale wenye hela za maana; wanaweza kuwa wamesoma huko UDSM ama chuo chochote na wanaweza kuwa hawakusoma kabisa!. Kujidhania una akili za kufaulia mitihani halafu usiwe na hela za maana(au angalau za kutosha) huo ni ujuha."

Akiwa bado anashangaa-shangaa nilichomwambia, nikamuongezea; "Kwanza wanaohangaika na CV za mavyuo ni wale wanaotaka kuwavutia wenye akili (waajiri) ili wawaelekeze cha kufanya(yaani wawaajiri). Mtu mwenye maono ya kujiajiri hahangaiki na CV za mavyuo bali anaangalia maarifa ya kumsaidia na kimsingi anaweza hata asiende shule bali akayapata maarifa hata mtaani tu". Akaniuliza, "Unamaanisha nini?"

Nikamjibu swali lake:- "Brother umesoma chuo Kikubwa lakini bado una akili za kikoloni zinazowaza kuwa hakuna maisha ya maana mpaka uajiriwe. Kusoma ni jambo zuri na kuajiriwa sio jambo baya lakini usikariri kuwa hakuna maisha pasipo kuajiriwa; na usifikiri kila anaefika chuo kikuu anawaza kuajiriwa tu”. Yule brother alipaniki nusura anizabe makofi, nikaamua kuondoka "fasta" na kiukweli nilimchanganya na kumuudhi sana. Unajua ni nini? Ngoja nikupe pointi tatu fasta fasta:-

1. Siku hizi mafanikio kimaisha hayamo katika CV ya chuo ulichosoma na kamwe hutatajirika (au angalau kuwa na pesa za maana) kwa kutegemea mshahara pekee". Ikiwa imepita miaka saba sasa, sijajua hali ya kiuchumi na kimaisha ya yule brother; lakini ikiwa hajabadilisha ile "mentality" nina uhakika atakuwa "ni mbangaizaji tu" kiuchumi na kimaisha kwa ujumla licha ya kuwa anamiliki cheti cha digrii kutoka nchi ya ng'ambo!

2. Hili ni tatizo lililopo miongoni mwa wasomi wetu wengi, wanachanganya nafasi ya maarifa na vyeti. Kwao kumiliki cheti cha ngazi fulani kutoka chuo fulani, ni muhimu zaidi kuliko ubora wa maarifa anayokuwa nayo kichwani. Vijana wanatakiwa kutambua kuwa muundo wa soko la ajira umebadilika sana, soko la ajira linazingatia uwezo wa muhitimu kushinda jina la shule ama chuo alichosoma muhitimu.

3. Nimekuwa nikiwaeleza wasomi kwamba, “Ukishamaliza kazi ngumu ya kujifunza "profeshino" yako; iwe ni ualimu, udaktari, uanasheria, uinjinia, n.k; basi ni vema usisahau pia kujifunza jinsi ya kutafuta hela. Kupata hela za kawaida kupitia mshahara utazipata tu; kwa; hiyo "profeshino", ila kwa "case" ya kuwa na hela za kutosha itakulazimu ujifunze mtaala mwingine mbali na hiyo "profeshino". Kwa sababu "profeshino" bila kuwa na hela za kutosha ni mzigo” #SmartMind

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top