Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: MH. EDWARD LOWASSA ANGURUMA KATIKA UFUNGUZI WA KIKAO CHA BAVICHA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
* MH. EDWARD LOWASSA ANGURUMA KATIKA UFUNGUZI WA KIKAO CHA BAVICHA * Awali ya yote aliwashukuru wajumbe Wa Baraza la vij...

*MH. EDWARD LOWASSA ANGURUMA KATIKA UFUNGUZI WA KIKAO CHA BAVICHA *




Awali ya yote aliwashukuru wajumbe Wa Baraza la vijana CHADEMA kwa kufika, akiwapongeza kwa kufanya kazi kubwa ya kusimamia uchaguzi na kulinda kura kwa jasho na damu .Pia aliwapongeza BAVICHA kwa kutii maelekezo ya Mkt. Freeman Mbowe ya kutokwenda Dodoma na kukaa na kujadili namna mbadala za kupigania demokrasia na utawala bora akiwasisitiza kuwa Ujumbe umefika kwa watawala.


*MAMBO MAKUU ALIYO ZUNGUMZA NA KUSISITIZA YALIKUWA KAMA IFUATAVYO*


*1. MIKUTANO YA HADHARA *


Mh. Edward Lowassa alisema; CCM watakapo maliza kumchagua Mwenyekiti wao wa Taifa watalazimika kufanya mkutano wa kumtambulisha ,hivyo hana shaka CCM na jeshi lao la Polisi wataruhusu mikutano ya hadhara maana watataka kufanya mikutano hio ya hadhara ya kumtambulisha Mwenyekiti wao . Alienda Mbali zaidi na kusema kuwa hivi karibuni IGP alipo kuwa anahojiwa na Tido Mhando  alionyesha wazi kuruhusu mikutano ya Hadhara .


*2. VIJANA NI CHACHU YA MABADILIKO*


Mh. Edward lowassa alisema vijana wasione Aibu katika kupambania nchi yao , angewashangaa sana kuona wapo kimya wakati demokrasia inakandamizwa akitolea mfano yeye akiwa kijana alifanya hivyo Mara kadhaa chini ya uongozi Wa Baba Wa Taifa Hayati Mwl .Julius Nyerere nyakati hizo na Baba wa Taifa hakuwazuia bali aliwaongoza katika mambo kadhaa walio kuwa wakiteleza maana vijana ni chachu ya mabadiliko ,lazima vijana wapewe nafasi ya kuleta mawazo mapya alisisitiza .


*3. KUHUSU AJIRA*


Mh. Edward lowassa amesema anasikitishwa kuona vijana wanatengwa katika AJIRA ,vijana walioamua kuwa wapinzani wanatengwa katika ajira ikiwa wao ni raia halali wa nchi hii ,Alisema ni ajabu sana kuona vijana wa upinzani hawapewi nafasi za ajira katika teuzi za RC,DC ,DED na DAS ikiwa nafasi hizi za usimamizi zinahusisha utaalamu ambao pia wao wanao bila shaka hata kuzidi wengi wao walio teuliwa. "Taifa hili ni letu sote bila kujali vyama vyetu, uteuzi wa kibaguzi ni jambo la kukemea kabisa, haki ya vijana kupata ajira ni ya wote bila kuangalia wanatokea vyama gani, kanda, ipi, rangi au makabila yao", Alisema.



*4. KUHUSU UMOJA WA KITAIFA NA MATUMAINI*

Amesisitiza umoja wa kitaifa; historia ya taifa letu ilijengwa na waasisi kwa umoja wa kitaifa bila aina yeyote ya ubaguzi .Pia amesema watanzania wamepoteza matumaini. Mh. Edward Lowassa alisema, Binadamu yoyote huishi kwa Matumaini, Lakini mambo yanayo endelea kwenye Taifa letu kwa sasa hayaleti matumaini. "Leo hii wananchi wanasema *maisha ya Mtanzania ni pasua kichwa*" kwa kuwa Matumaini wanapewa kundi la watu flani tu huku akitoa mfano wa mwaandishi mashuhuri wa Afrika, Chinua Achebe; alipoulizwa je utaondoka nchini kwako (Nigeria), alijibu "siondoki, hapa ndio Mungu aliponipangia kuishi".




*5. KUHUSU USHINDI WA UCHAGUZI MKUU 2020*


*"Im a longterm opportunist" Mh Edward Lowasa alisema; Uchaguzi mkuu ujao CHADEMA /UKAWA itashinda. Amesema ushindi wa uchaguzi ujao utatokana na mambo makuu manne kama ifuatavyo :

*A.Umoja ndani ya Chama na jumuia zake*, ikiwa kuwapa imani viongozi wake .
                
*B. Kukataa kwa namna yeyote ile jitihada za dola na CCM za kuwatenganisha miongoni mwao* , usalama wa Taifa ni waajiriwa Wa serikali lakini moja ya kazi zao ni kuwafitinisha vyama vya upinzani. Hivyo ni jukumu la wanachama kukilinda chama na kumlinda Mkt Mbowe alisisitiza. Alitoa mifano ya viongozi kama Mobutu Seseko wa Jamuhuri ya Kongo na Silvio Berlusconi wa Italia walivyotumia Usalama wa Mataifa yao na vyama vidogo vidogo vya upinzani kushika dola kwa kuwapa nguvu ya fedha ili wakose umoja.
                    
*C. "UKAWA ni lazima ulindwe kwa namna yeyote ile*, CUF ,NLD na NCCR wanaihitaji CHADEMA na CHADEMA wanavihitaji vyama Rafiki vya UKAWA kwa uwiano sawa" Mh Edward alisisitiza.
                         
*D. "Lazima vijana na wanachama wote twende Vijijini* kwa muda wa miaka 3,tukajenge chama katika misingi vijini walipo watu", kwa lugha ya kiingereza alisisitiza  “lets go back where people they are" . Alitolea mfano Mwaka 1987 ambapo Mwl Nyerere alipostaafu serikalini aliwauliza nini niwasaidie kipindi kile cha chama kimoja na wakajibu tusaidie kujenga chama , "Mwl Nyerere akazunguka Vijijini ndani ya mikoa 30 na yeye (lowassa alimsindikiza kwa mikoa 17 ,huko walizunguka Vijijini kujenga chama katika mashina ,walikutana na wanachama na kuwafanya wanachama wazungumze , CCM imepoteza mvuto hivyo wanapumulia mashine ambayo ni kazi ya Mwl 1987" Mh Edward lowassa alisema ..


Mwisho aliwashukuru kwa kuja na kuwatakia mijadala mema na maandalizi mema ya kushika dola 2020, akiwasisitiza kwa msemo mpya kwamba *"CCM imekosa mvuto, Mvuto upo CHADEMA"*

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top