Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: Viongozi wa dini mkoani KAGERA wameshauriwa kuimarisha ulinzi katika nyumba za ibada
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Viongozi wa dini mkoani KAGERA wameshauriwa kuimarisha ulinzi katika nyumba za ibada ili kuepusha vitendo vya wizi  vinavyojitokeza wakati w...
Viongozi wa dini mkoani KAGERA wameshauriwa kuimarisha ulinzi katika nyumba za ibada ili kuepusha vitendo vya wizi  vinavyojitokeza wakati wa ibada.

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani KAGERA ABEL MTAGWA ameyasema hayo kufuatia wizi wa pikipiki yenye namba za usajili MC 347ADP aina ya SUNLAGE inayomikiwa na BENEDICTO KAMUGISHA ilipoibiwa wakati ibada ikiendelea katika kanisa la Kiinjili la kirutheri Bukungu kata ya Kamachumu wilayani Muleba.



Kamanda MTAGWA amesema kuwa upelelezi na  uchunguzi wa tukio hilo unaendelea wa kubaini nani iliiba pikipiki hiyo.


Aidha amewataka viongozi wa makanisa kuajili walinzi wenye ueledi na kazi hiyo ili kupunguza changamoto za wizi zinazojitokeza.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top