Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WANANCHI WAHAKIKISHIWA UMEME WA REA KUFIKA KWENYE KILA KITONGOJI
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Wananchi   wilayani  Karagwe wametakiwa  kuendelea  kuvuta  subira  wakati  jitihada za  kufuatilia  vitongoji  na  vijiji  ambayo havik...

Wananchi   wilayani  Karagwe wametakiwa  kuendelea  kuvuta  subira  wakati  jitihada za  kufuatilia  vitongoji  na  vijiji  ambayo havikupata  umeme  wa  Rea   zinaendelea  kufanyika  ili  kuhakikisha  awamu  ya  tatu  inayofuatia  vinapata  umeme  huo.

Kauli  hiyo  imetolewa  na  mbunge wa  Jimbo  la  Karagwe  Innocent  Bashungwa  katika  mikutano  ya  hadhara  ya  kuwashukuru  wananchi  kumchagua  pia   kuwapa  mrejesho  wa  masuala mbalimbali  ya maendeleo  alizoshghulikia  kwa  nafasi  yake  ya  uwakilishi  wa  wananchi  Bungeni.

Amesema  wizara  ya  Nishati  na  madini  kupitia  mradi  wa  umeme  vijijini  tayari  wamemuhakikishia  kuwa  vitongoji  na  vijiji  vyote  ambavyo  havikupata  umeme  huo   kwa  awamu  zilizopita  hivyo  akasema  kuwa  tayari  ameorodhesha  vitongoji  na  Vijiji  vilivyokosa  umeme  huo  na  vimeisawailishwa  kwa  waziri  wa  wizara  husika.

Katika  hatua  nyingine  Innocent  Bashungwa  amesema  mradi  wa  maji  wa  Rwakajunju  tayari  umetengewa  fedha  katika  bajeti  ya  mwaka 2016/2017  zimetengwa  dolla  million  30  ambazo ni    sawa na  shilingi   billion  65  fedha  za  kitanzania  na  kusema  ukikamilika  utakuwa  ni  mkombozi  kwa  wananchi.

Mtendaji  wa Kata  ya  Bweranyange Niclous  Rubambura    akisoma  taarifa  ya  Kata  amesema  kuwa  inakabiliwa  na  changamoto  ya  kutokuwa  na  watendaji  wa  vijiji hali  inayosababisha  kazi   za  kuwaletea  maendeleo  kwa  wananchi  kukwama.

Amesema  kata  hiyo  ina  vijiji  4  lakini ni  vijiji  vitatu  havina  watendaji  na  kijiji  kimoja  cha  Chamchuzi  mtendaji  wake  ni  mgonjwa  wa  muda  mrefu  hivyo  ni  changamoto  kubwa.

Wananchi  wa  vijiji vya  kata  ya  Bweranyange  wamesema  kuwa  ili  kasi  ya  maendeleo  iwepo ni  lazima  watumishi  waliopo  wasipewe  majukumu  ambayo  siyo  utalaamu  wao kwani  waliokaimu  vijiji wengi  wao  ni  walimu.

Akijibu  hoja  hizo  Mbunge  wa  jimbo  la  Karagwe Innocent  Bashungwa  amesema  kuwa  changamoto  za  upungufu  wa  watumishi  katika  wilaya  ya  Karagwe  anazitambua.

Hata  hivyo  amewataka  wananchi  kuchangamkia  fursa  ya  kuwa  jirani  na  Nchi  ya  Rwanda  na  nchi  hiyo  imeanzisha  kiwanda  cha  kutumia  mihongo  hivyo  wananchi  wakalime  kwa  wingi  mihogo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top