Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: KESHO SHUGHULI ZOTE ZA KIJAMII KARAGWE KUSIMAMA MUDA WA SAA 4 KUPISHA USAFI
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu  wa  wilaya  ya  Karagwe  Godfrey  Muheluka  amewataka  wananchi  wilayani  Karagwe  kuhakikisha  maeneo  yao  yote  yanakuwa  safi  w...
Mkuu  wa  wilaya  ya  Karagwe  Godfrey  Muheluka  amewataka  wananchi  wilayani  Karagwe  kuhakikisha  maeneo  yao  yote  yanakuwa  safi  wakati  wote  na  kesho  Alhamisi  itakuwa  ni  siku  maalumu  ya  uzinduzi  wa  ukaguzi  wa usafi  wa  mazingira.



Ametoa  agizo  hilo  leo  katika  kikao cha  kamati  ya  Huduma  za  Afya  ya  Msingi  PHC wilaya  ya  Karagwe  kilichofanyika  katika  ukumbi  wa  ofisi  ya  mkuu  wa  wilaya  ya  Karagwe baada  ya  kupewa taarifa  ya  kusuasua  kwa  hali  ya  ushiriki  wa  wananchi  kufanya  usafi.



Muheluka  amesema  kuwa utaratibu  wa  kufanya  usafi  unafahamika  hivyo  kinachotakiwa  ni  kukagua  maeneo  yote  na  kuwataka  viongozi  kuanzia  ngazi  ya  vitongoji  hadi  wilaya  kuhakikisha  maeneo  yote  yanakuwa  safi  wakati  wote.


Amesema  kwa  siku  ya  Kesho  Agosti 11 shughuli  zote  hatafanyika  kuanzia  saa  moja  hadi  saa  nne  asubuhi  itakuwa  ni  usafi  hivyo  huduma  za  ofisi  na  maeneo  ya  biashara  zitaanza  saa  nne   hivyo  watu  wote   wakashiriki usafi  na  atakayekutwa  eneo  lake  ni  chafu  faini  yake  ni  shilingi  laki  moja au  kifungo  cha  miezi  sita  au  vyote  kwa  pamoja.




Hata  hivyo  amewataka  wajumbe  wa  kamati  ya  Huduma  za  Afya  ya  Msingi  PHC wilaya  ya  Karagwe  kuripoti  ofisini  kwake  bila  kukosa  ili  zoezi  la  ukaguzi  liweze  kuanza  mara  moja.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top