Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: KULA MLO KAMILI NA KUFUATA MASHARTI YA LISHE KUNAWEZA KUPUNGUZA UHARIFU NCHINI
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Zikiwa zimebaki siku chachee kuazimisha siku ya kunyonyesha duniani wanawake wilayani Missenyi wameshauriwa kula mlo kamili pamoja na kunywa...
Zikiwa zimebaki siku chachee kuazimisha siku ya kunyonyesha duniani wanawake wilayani Missenyi wameshauriwa kula mlo kamili pamoja na kunywa maji mengi katika kipindi cha mimba.

Afisa lishe wilayani MISSENYI ZAINATI JAWADU ametoa kauli hiyo wakati akiongea na vyombo vya habari juu ya wito kwa wanawake wote kabla ya kuadhimisha siku ya unyonyeshaji.

ZAINATHI amesema kuwa mlo kamili kipindi cha mimba ni matokeo ya kuzaa mtoto mwenye  afya pamoja na kupunguza magonjwa mbalimbali pale mtoto anapozaliwa.

Akiongelea kipindi mtoto anapozaliwa amesema kuwa maziwa ya kwanza baada ya saa moja kujifungua ni maziwa muhimu na yana virutubisho ambavyo uwezi kuvipata katika maziwa yeyote.

Aidha amewataka wanawake kujiamini pindi wanapojifungua kuwa wanauwezo wa kuwanyonyesha watoto wao bila maziwa kupotea mpaka miezi sita huku akiwataka wanawake waliojiriwa kuacha tabia ya kuwaacha watoto wachanga muda mrefu bila kuwanyonyesha

..

Hata hivyo ametoa wito kwa wazazi walezi kuwapa watoto wadogo samaki ambapo amesema kuwa mafuta yanayopatikana kwenye samaki hayawezi kupatikana katika kitoweo chochote.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top