Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: MKUU WA WILAYA YA BUKOBA AFANYA ZIARA YA KUSHUTUKIZA KATIKA MRADI WA MAJI KUONA KAMA ALIUZIWA MBUZI KWENYE GUNIA WATENDAJI
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa Wilaya   ya Bukoba   Deodatus Kinawilo afanya ziara ya kushutukiza katika Kata Nyakibimbili Kijijini Kitahya Halmashauri ...




Mkuu wa Wilaya  ya Bukoba  Deodatus Kinawilo afanya ziara ya kushutukiza katika Kata Nyakibimbili Kijijini Kitahya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba  Agosti 9, 2016 katika chanzo cha maji kilichopo kijijini hapo ili kuhakiki kama pampu ya kusukuma maji  kama ilifungwa na ipo katika tenki la maji lilojengwa katika chanzo hicho cha maji.










Mkuu huyo wa Wilaya aliamua kufanya ziara hiyo ya ghafla na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama mara baada ya kuletewa malalamiko na wananchi kuwa siku mradi huo ulipowekewa jiwe la msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima Julai 27, 2016 maji yaliyotoka katika ghati la Ibwera yalijazwa kwenye tenki na gari la kubebea maji  kwani pampu ya kusukuma maji haikuwepo katika tenki lilipo kwenye chanzo cha maji.



Baada ya kufika katika chanzo hicho cha maji Kinawilo aliyeongozana pia na Kaimu  Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba  Gregory Fabian,  Mhandisi wa Maji  Dismas Martin, na Mhandisi Mshauri wa Mradi huo Mwesiagwa Mtagaywa wa Kampuni ya (O & A Company Ltd.) alikagua mradi huo na kugundua kuwa pampu ipo na inafanya kazi vizuri ya kusukuma maji.


Aidha, iligundundulika kuwa maji mara baada ya  kusukumwa kutoka kwenye tenki  umbali wa mita 22 kutoka kwenye tenki hilo bomba limekatika kiungio jambo linalosababisha maji kutopanda hadi katika Kata ya Ibwera ambapo Mhe. Kinawilo alimuagiza Mhandisi Mshauri kuhakikisha anamshauri Mkandarasi kufanya marekebisho ya haraka nadani ya wiki moja.
Aidha , katika mradi huo kuliibuliwa suala la wananchi kukata mabomba ya maji katika chanzo hicho na kusababisha maji kutoenda katika tenki linalohudumia vijiji vitatu vya Kitahya, Kibona na Itongo na kusababisha Diwani wa Kata ya Nyakimbimbili Haji Matsawilly Juma kulalamika kuwa maji hayawafikii wananchi na kumwomba Mkuu wa Wilaya kumhimiza Mkandarasi kumaliza kazi ili maji yatoke kwa wananchi kama ilivyotarajiwa.


Maagizo,  Kinawilo baada ya kushuhudia uharibifu huo alimwagiza Mhandisi Mshauri kuhakikisha Mkandarasi anafunga vifaa vyenye ubora ili thamani ya vifaa iendane na gharama za mraddi huo. Pili alimwagiza Mwenyekiti wa Kijiji Kitaya   Bw.Johnstone Kahigwa aliyedai kuwa kijiji hakikukishirikishwa tangu mwanzo wa mradi kuhakikisha anashirikiana na Halmashauri ya kijiji chake kuilinda miundombinu ya mradi huo kwa sababu mradi upo katika eneo lake.



Vilevile  Kinawilo alimwagiza Mhandisi Mshauri kuhikikisha anfanya marekebisho yote ya mradi huo ndani ya wiki moja ili wananchi waanze kupata huduma ya maji. Na mwisho aliwaagiza Watendaji wa Kata za Ibwera na Nyakibimbili kuititsha mkutabno wa pamoja kwa kamati za maji za Vijiji vya Kitaya, Kibona,Itongo na Ibwera ili kuweka mikakati ya kuilinda miundombinu ya mradi huo wa maji.


Mradi huo wa maji ukikamilika unatarajiwa kuhudumia vijiji vinne vya Kitaya, Kibona,Itongo  (Kata Nyakibimbili)na Ibwera (kata Ibwera) una gharama ya zaidi ya shilingi milioni 430 na ulianza katika awamu ya kwanza mwaka 2009 katika upembuzi yakinifu na usanifu, aidha utekelezwaji wake ulianza rasmi  katika awamu ya pili iliyoanza Mwezi Julai, 2013.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top