Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: NAIBU WAZIRI MHANDISI STELLA MANYANYA ATOA AHADI YA BWENI LA KISASA KUJENGWA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
      NAIBU waziri wa elimu sayansi na teknolojia mhandisi Stella Manyanya ameahidi kujenga bweni moja la kisasa na kutoa vitanda 100...


      NAIBU waziri wa elimu sayansi na teknolojia mhandisi Stella Manyanya ameahidi kujenga bweni moja la kisasa na kutoa vitanda 100 katika shule ya sekondari Bugene ambayo ina kidato cha tano na sita.

    Hayo yalisemwa jana na mhandisi manyanya alipokuwa katika chuo cha ufundi cha halmashauri ya wilaya ya karagwe,Karagwe District Vocational Training Center (KDVTC) baada ya kupokea taarifa ya elimu ya wilaya ya karagwe na kukagua miundombinu ya chuo hicho.

   “Niliwahaidi tu kwamba tayari wizara imejikomiti kujenga bweni zuri la kisasa na kuweka vitanda 100 katika bweni hilo ili kuongeza molali kwa wanafunzi wanaosoma katika shule ya Bugene lakini pia ikizingatiwa kwamba wilaya hii ipo mpakani na shule za nchi hizo ni nzuri ”alisema mhandisi Manyanya

   Akisoma taarifa ya wilaya afisa elimu sekondari wilaya ya karagwe Upendo Rweyemamu alisema kuwa halimashauri ya wilaya hiyo ina shule moja ya sekondari ya Bugene ambayo ina kidato cha sita.kati ya shule 25 za sekondari za serikali na inachangamoto mbalimbali ikiwemo  pamoja na upungufu wa mabweni ya wasichana na wavulana na vitanda vipatavyo 120.

    Rweyemamu alieleza kuwa halimashauri ililenga kupokea wanafunzi 90 ikiwa ni wavulana 45 na wasichana 45 kidato cha tano katika shule ya Bugene na kwamba waliopangwa walikuwa 160 wakiwemo wavulana 80 na wasichana 80 hadi tarehe 5 agosti mwaka huu walikuwa wamepokelewa wanafunzi 125,wavulana 66 na wasichana 59.

  Alitaja hali ya miundo iliyopo shuleni hapo kuwa ni pamoja na bweni moja  la wavulana na bweni moja la wasichana ,umeme,bwalo na vyumba vya madarasa changamoto nyingine alizitaja kuwa ni vitanda 120 na vitanda 30 viliazimwa kutoka kituo cha afya kayanga na vitanda 60 vimeanza kutengenezwa.

   Kwa upande wake mwenyekiti wa halimashauri ya wilaya ya karagwe Walles Mashanda  alimpongeza naibu waziri kwa kitendo chake cha kuonyesha nia ya kujenga bweni la kisasa na vitanda katika shule hiyo huku akimuomba kuongezewa walimu katika shule za msingi kwa kuwa wilaya hiyo ina upungufu wa walimu 834 na mwaka jana walipata walimu saba tu!.

   Aidha Mashanda alimuomba mhandisi Stella manyanya kutatua changamoto ya walimu wa sayansi kwani halimashauri ya wilaya ya karagwe inakabiliwa na upungufu wa walimu wapatao 87,ambapo alisema kuwa wilaya inahitaji walimu wa sayansi wapatao 169 na waliopo ni 82.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top