Unknown Unknown Author
Title: WAFANYABIASHARA WAILALAMIKIA JUMUIA YA UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA ( CCM)
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
BAADHI ya wafanyabiashara wa maduka katika jengo linalomilikiwa na umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wilayani Karagwe mkoani Kagera wameu...

BAADHI ya wafanyabiashara wa maduka katika jengo linalomilikiwa na umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wilayani Karagwe mkoani Kagera wameulalamikia umoja huo kufunga vyumba vyao bila kufuata utaratibu wa kisheria na kuuathiri uchumi wao.


Hayo yalibainishwa jana na baadhi ya wafanyabiashara hao katika mji mdogo wa Kayanga wilayani humo wakati zoezi la kufunga maduka yao likifanyika kwa kuendeshwa na umoja huo kwa kusimamiwa na jeshi la polisi  kwa madai kuwa ni kutokana na wafanyabiashara hao kutolipa kodi ya pango kwa kipindi kirefu.


Mmoja wa wafanyabiashara hao Grace Mahumbuka ambaye pia ni mwenyekiti wa umoja wa wanawake wajane wilayani humo alisema kuwa taratibu za kufunga maduka yao hazikufanyika kisheria zaidi kwani wenye maduka hawakushirikishwa, mali zao hazikuhesabiwa wala hakuna mwenyekiti wa mtaa aliyeshirikishwa.“zoezi hilo lilifanyika kwa jaziba zaidi na lililenga kutuathiri kiuchumi na zaidi zaidi ilikuwa ni kuwakomoa wale ambao hawakukiunga mkono chama cha mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mkuu mwaka jana” alisema Mahumbuka.


Alisema kuwa baadhi yao wameathirika  na zoezi hilo kutokana na wafanyabiashara walioingia mkataba na (UWT) kuwatoza hela za kodi na kutowalipa (UWT) suala ambalo limepelekea wao kufungiwa maduka bila taarifa.


Aliongeza kuwa kwa kuwa kitendo hicho wamekichukulia kama cha udhalilishaji kwao, kilicholenga kuwaathiri kiuchumi na kisaikololojia wanajipanga kufungua kesi mahakamani kudai haki yao.


Kwa upande wake mwenyekiti wa (UWT) wilaya ya Karagwe Rehema Mtawala alisema kuwa katika zoezi hilo wafanyabiashara saba ndio walaliolipa shilingi milioni tano na kuruhusiwa kuendelea na biashara zao kila mmoja ambapo deni lililobaki kwa wafanyabiashara wengine ni shilingi milioni 8.Hata hivyo aliongeza kuwa umoja huo unatarajia kuwafikisha mahakamani wafanyabiashara wengine ambao bado wamegoma kulipa fedha hiyo kwani tayari walishapata notisi ya kuhama iliyotolewa na dalali wa mahakama wilayani humo (court brocker) na kuwataka kutolichukulia suala hilo kama la kisiasa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top