Baraza la Madiwani
katika halamashauri ya wilaya ya Misenyi wameiomba halmashauri ya Misenyi kwa
kushirikiana na serikali kuu kumalizia miradi ya maendeleo ambayo haikumalizika
katika mwaka wa fedha 2015/2016.
Wakiwasilisha taarifa zao za utekelezaji wa miradi
ya maendeleo katika kata zao mbele ya mwenyekiti wa halmashauri hiyo
kipindi cha APR-JUN madiwani hao wamesema kuwa licha ya kuanza mwaka mpya wa
fedha bado kunaviporo vingi vya miradi ya maendeleo ambavyo havikutekelezwa.
Miradi mikubwa ambayo iliwekwa kwenye bajeti na
haikutekelezwa kwa asilimia kubwa ni pamoja na miradi ya ukarabati wa barabara
zinazounganisha kata na vijiji ,miradi ya maji pamoja na ukarabati wa miundo
mbinu hasa katika nyumba za walimu ,shule na vituo vya afya.
Akizungumzia swala la ukarabati na utengenezaji wa
barabara katika kata mbalimbali za
halmashauri ya Missenyi mwenyekiti wa halmashauri hiyo PROJESTUS TEGAMAISHO
amesema kuwa barabara zote zilizotengewa bajeti kupitia mfuko wa CBJ mfuko huo
haukuleta fedha za barabara.
TEGAMAISHO amesema kuwa kutokana na viporo muhimu
kutotekelezwa katika bajeti iliyopita wataendelea kushughulikia miradi hiyo na
kuibua upya ili kuwaondolea wananchi adha inayowakabili.
Baadhi ya changamoto nyingine zilizotajwa na
madiwani katika kata zao ni upungufu wa watumishi hasa maofisa watendaji wa
vijiji upungufu wa madawa katika vituo vya afya upungufu wa walimu wa sayansi
na upungufu wa nyumba za walimu na vyumba vya madarasa.
Post a Comment