Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: CRDB BANK KARAGWE YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO AFRIKA KWA KUTOA ZAWADI KWA SHULE
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Benki ya CRDB tawi la Karagwe imetoa zawadi ya mashine ya kudurufu (Photocopy mashine) yenye thamani   ya   shilingi million   ...




Benki ya CRDB tawi la Karagwe imetoa zawadi ya mashine ya kudurufu (Photocopy mashine) yenye thamani  ya  shilingi million  tatu kwa shule ya msingi Kayanga  ikiwa  ni  sehemu  ya  maadhimisho  ya  mtoto  Afrika  ambayo  hufanyika Juni 16  kila  mwaka  Afrika  nzima.

Zawadi hiyo imetolewa leo na uongozi wa CRDB tawi la Karagwe kwa lengo la kuchochea  ufaulu mzuri kwa wanafunzi wa shule hiyo na hatimae waweza kufikia malengo yao.

Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Karagwe Jeremiah  Msemo amesema zawadi hiyo imetolewa na benki  yake  kwa shule hiyo,ni  motisha kwa walimu  na  wanafunzi  hao  ili  waweze  kuongeza  ufaulu kwenye  masomo yao.


Msemo amesema anaamini kupitia zawadi hiyo iliyotolewa itasaidia  wanafunzi kufikia  malengo yao na kusema   kuwa  ni jukumu la  wazazi na walezi kushirikiana na walimu ili kuinua ufaulu wa wanafunzi hao.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kayanga mwalimu  Osward Marcel amesema kutokana na zawadi hiyo iliyotolewa shuleni hapo anaamini ufaulu wa wanafunzi hao utaongezeka kutoka asilimia 91 na kufikia asilimia 100.


Katika hatua nyingine benki ya Crdb tawi la Karagwe imesherekea siku ya mtoto wa Afrika na watoto mbali mbali kutoka maeneo tofauti wenye akaunti na wasio na akaunti ya watoto iitwayo Junior Jumbo katika benki hiyo.


Kupitia maadhimisho hayo Meneja wa Benki ya Crdb tawi la Karagwe Jeremia Msemo amewataka wazazi na walezi wa watoto wote kuwafungulia akaunti watoto wao katika benki ya Crdb kwa ajili ya kuwajengea tabia ya kutunza akiba wakiwa wadogo na baadae kuwawezesha kufikia malengo yao mbali mbali ya baadae.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top