Mvua iliyoambatana na
upepo mkali iliyonyesha
jana jioni kata ya Kibale
Wilayani Kyerwa imesababisha madhara
makubwa na kuaribu takribani ya hekali 200 za mazao ya chakula zikiwemo zaidi
ya nyumba 70 kuezuliwa na upepo.
Akizungumza na MTANDAO HUU Diwani
wa kata hiyo Sadati Katembala amesema mvua hiyo iliyonyesha kwa dakika 20
imeharibu migomba ,mihogo na maharage hususani vitongoji vitano vilivyomo
kwenye kata hiyo ambavyo vimeathilika zaidi na kusababisha wanachi kukosa mahali pa kulala usiku wa kuamkia leo.
Kwa upande wao waathilika wa mvua
hiyo wakizungumza na Chombo hiki wamesema hali hiyo imewarudisha nyuma
kimaendeleo kwani wengi wao wataanza upya kulima mazo na wengine ujenzi wa
nyuma zao.
Linusi Colosper ambaye ni mfanya biashara wa bidhaa
mbalimbali,amesema amepata hasara kubwa kwani mvua hizo zimeharibu bidhaa zake
zilizokuwa ndani ya nyumba ambayo imeezuliwa na upepo huo huku baadhi yao wakiendelea
kuangaikia sehemu za kujihifadhi.
Hata hivyo Diwani wa kata hiyo
amesema taarifa zimefikishwa wilayani na kuweza kufanya tathimini ya jumla ya
maafa yaliyosababishwa na Mvua hiyo ili serikali iweze kutoa msaada wa haraka
kwa wakazi hao .
Post a Comment