Timu
ya Taifa ya Chad ‘Les Sao’ imejiondoa katika michuano ya kuwania
kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) itakayofanyika mwaka 2017 nchini
Gabon.
Taarifa
ya kujitoa kwa Chad imetolewa na Shirikisho la Mpira wa miguu barani Afrika
(CAF) leo baada ya Les Sao kuandika barua ya kujitoka katika mashindano hayo
ikiwa katika kundi G pamoja na timu za Tanzania, Nigeria na Misri.
Chad
ilitarajiwa kucheza kesho Jumatatu dhidi ya Tanzania katika uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam, ikiwa ni mchezo wa marudiano wa kundi G baada ya kucheza
mchezo wa awali jijini N’Djamena katika ya wiki.
Katika
mchezo wa awali uliochezwa uwanja wa Idriss Mahamat Ouya, Taifa Stars iliibuka
na ushindi wa bao 1- 0 , bao lililofungwa na nahodha Mbwana Samatta dakika ya
30 ya mchezo.
Kufuatia
kujitoa kwa Chad, matokeo ya michezo yote iliyoihusisha timu hiyo yanafutwa, na
msimamo wa kundi G kwa sasa unaongozwa na Misri yenye pointi 4, Nigeria pointi
2 na Tanzania pointi 1.
http://tff.or.tz/news/392-chad-yajitoa-afcon-2017
Post a Comment