Mrajisi wa
vyama vya ushirika
Tanzania ameivunja rasmi
bodi ya chama
kikuu cha ushirika
cha wilaya za
Karagwe na Kyerwa
cha Karagwe District
Cooperative Union Ltd(KDCULTD) kwa tuhuma
mbalimbali ikiwemo ubadilifu
wa pesa kiasi
cha shilingi 1.3 billioni na
baadhi ya wajumbe kukiuka sheria
namba 6 ya
ushirika ya mwaka 2013
Uamuzi huo umetolewa
leo na Doroth
Kalikamo ambaye alimwakilisha
mrajisi wa vyama
vya ushirika Tanzania
katika mkutano mkuu
wa 29 wa kawaida
wa KDCU LT wa kupitisha
makadirio ya bei
ya msimu 2016/2016
uliofanyika katika ukumbi
wa CCM Kayanga.
Amesema kuwa
kutokana na tuhuma
zilizobainiwa na mkuu
wa wilaya ya
Karagwe Deodatus Kinawiro
kuwasilisha ripoti kwao
waliona zina ukweli
lakini na mrajisi
alifanya uchunguzi wake
ikabainika hizo zina
ukweli na sheria
ya ushirika ilikiukwa na
kuisababishia KDCU LTD
kupata hasara.
Kalikamo amebainisha
kuwa makosa yaliyobainiwa
katika uchunguzi huo
kuwa ni kuwepo
ubadilifu wa kiasi
cha shilingi 1.3 billioni
za mauzo ya
msimu 2013/2014 na
fedha zake kupatikana
mwaka 2015,nyingine ni wajumbe
wa bodi hiyo
kuuza kahawa bila
kushindanisha hivyo kuuza
(Direct sells) na kukisababishia chama
hasara ya shilingi 900
milioni.
Ametaja makosa
mengine kuwa makamu
mwenyekiti wa bodi
ya KDCU LTD Daudi
Magayane alidanganya wakati
wa kujaza fomu
za kuwania nafasi
hiyo kwani imegundulika
aliwahi kuhukumiwa kifungo cha
miaka 5 na kutumikia
mwaka mmoja kabla
ya kutoka kwa
rufaa pia alikuwa
askari Magereza alifukuzwa
kazi wakati sheria
ya ushirika inasema
usiwe umetumikia kifungo
au kuhukumiwa.
Aidha katika
mkutano huo ambao
umefanyika leo bodi
mpya ya watu
saba itakayodumu kwa
mwaka mmoja imepewa
jukumu la kusimamia udhibiti
wa matumizi na
kusimamia menejiment ili
kuokoa KDCU LTD
kwenye hatari ya
kufilisika.
Wajumbe wapya
wa bodi ya
KDCU LTD iliyochaguliwa kuongoza
kwa mwaka mmoja
ni Witness Kabyazi ,Peter Colonery, Anselimi Alphonce,Fridolin Faustine
Kasenene, na Ndayamukama Libenti
Wengine ni
Theobadi Mganga ambaye
amechaguliwa pia kuwa
mwenyekiti wa KDCU LTD
na Brighton Kaijage
amechaguliwa kuwa Makamu
mwenyekiti huku mwakilishi
wa bodi akichaguliwa
Witness Kabyazi.
Hata hivyo
bodi hiyo imechaguliwa
kufuatia iliyokuwepo kutuhumiwa
kwa ubadilifu wa
fedha na uchunguzi
wa tuhuma hizo
bado unaendelea kufanyika
chini ya vyombo
vya serikali vyenye
mamlaka hizo.




Post a Comment