Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella
amesema watendaji ambao maeneo yao yataendelea kukithiri kwa vitendo vya
uhalifu, migogoro ya ardhi, uharibifu wa mazingira na uchafu atawatumbua
majipu.
Akijibu swali aliloulizwa na
mwandishi wa habari mwishoni mwa wiki kuhusu kuibuka kwa vitendo vya uvamizi,
uporaji na mauaji katika jiji la Mwanza, alisema Serikali haitavumilia kuona
watu wasio na hatia wakipoteza maisha na mali zao huku wenye dhamana ya ulinzi
wakikaa bila kuchukua hatua.
Mongella alisema: “Sitasubiri
nitumbuliwe mimi, nitawatumbua kwanza viongozi na watendaji wazembe kabla
sijatumbuliwa.
“Kwa kipindi cha wiki mbili
nilichokaa Mwanza kumetokea matukio mawili ya wafanyabiashara ya maduka ya
fedha kwa njia ya mtandao kuvamiwa, kuporwa na wengine kuuawa kwa kupigwa
risasi, hii haikubaliki na siko tayari kushuhudia vifo vingine
Post a Comment