Wenyeviti wa vitongoji
pamoja na watendaji
wa mamlaka ya
mji mdogo wa Kayanga
wilayani Karagwe wametakiwa
kutafakari na kujadili
mambo yenye tija
kwa maendeleo ya wananchi
kuliko kuendelea kujadili
vitu vidogo ambavyo
havina maslahi kwa jamii
na Taifa.
Kauli hiyo imetolewa leo
na mkuu wa
wilaya ya Karagwe Deodatus
Kinawiro wakati akitoa
hotuba yake kwa
wajumbe wa baraza
la mamlaka ya
mji mdogo wa
Kayanga katika kikao
cha baraza hilo
kilichofanyika katika ukumbi
wa kituo rafiki
cha vijana maarufu
kama Angaza amesema
kuwa badala ya
kukaa na kujadili
masuala madogo yasiyokuwa
na tija kwa
jamii ni bora
wakajikita zaidi kwenye
mambo ya maendeleo
ambayo yanatija kwa
jamii na Taifa
kwa ujumla.
Amesema kuwa wajumbe
hao inabidi kujikita
zaidi kuweka mipango
ya kuendeleza mamlaka
ya mji mdogo
wa Kayanga utoke
kwenye mamlaka na
kuwa mji kamili pia
amebainisha masuala ya
mpango mji ,usafi wa
mji na mambo
mengine ya kuundeleza
inabidi kupewa kipaombele
cha kwanza katika
shughuli zao za
kila siku.
Kinawiro
amewataka pia wajumbe
hao ambao ni
wenyeviti wa vitongoji
vinavyopatikana kwenye mamlaka
ya mji mdogo
wa Kayanga kuwa wabadilike kifikira
na kuachana na utamaduni
wa kufanya kazi
kwa mazoea na
kuzingatia muda waliojiwekea
ili kuweza kufikia malengo
yao.
Mwenyekiti wa halmashauri
ya wilaya ya
Karagwe Walless Mashanda ambao
ni walezi wa mamlaka
ya mji mdogo
wa Kayanga amewashauri
wajumbe hao kujikita
kwenye mpango mkakati kwa
kuweka utaratibu wa
kukusanya ushuru kama
chanzo cha mapato
kitakachoendesha mamlaka ya
mji huo.
Amewataka pia kutoa
elimu ya ulipaji
kodi kwa wananchi haswa
wakazi wa mamlaka
ya mji mdogo
wa Kayanga kwa
kutumia mikutano ya
hadhara na kwa
kutumia vyombo vya
habari ili waweze kufikia lengo
la makusanyo kuliko
ilivyo sasa ambapo
mwaka wa fedha 2015/2016 walitakiwa
kukusanya million 213 lakini
mpaka sasa wamekusanya
million 8 tu sawa
na asilimia 3%ya makusanyo.
Kwa upande wake
mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya wilaya
ya Karagwe Mhandisi
Richard Ruyango amewataka
wajumbe wa baraza
hilo kuongeza kasi
ya makusanyo ili
waweze kupata fedha
za kuendesha mamlaka
ya mji mdogo
kwani kwasasa halmashauri
inakabiliwa na mambo
mengi ya matumizi
ya fedha.
Aidha katika kikao
hicho wajumbe hao
wameonesha kuridhishwa na
kitendo cha uongozi
wa halmashauri ya
wilaya kuhudhuria na
kutoa ufafanuzi wa
hoja kadhaa zilizokuwa
zinawasumbua kwa muda
mrefu na leo
kupatiwa ufumbuzi.
Hata hivyo katika
kikao hicho kilichokuwa
chini ya uenyekiti
wa mamlaka ya
mji mdogo wa
Kayanga Amos Kahwa
amewataka wajumbe kutekelezwa yote
yaliyoadhimiwa kwenye kikao
cha leo na kuwataka
kusimamia kwa karibu
shughuli za maendeleo
na haswa ukusanyaji
wa mapato ya mji mdogo
wa Kayanga.
Post a Comment