Wakulima wa zao la kahawa
Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera wametakiwa kuzingatia kanuni za kilimo
ili kuhakikisha wanavuna kahawa yenye ubora ambayo itawaongezea kipato chao.
Wito huo umetolewa na Afisa
kilimo anayeshughulika na zao la kahawa Wilayani Karagwe Cleophace Kanjagaile
leo wakati akiongelea kuhusu utunzaji wa
ubora wa kahawa.
Kanjagaile amesema wakulima
wa zao la Kahawa wakizingatia kanuni za kilimo wanazoelekezwa na wataalamu wa
kilimo anaamini zao hilo litakuwa la thamani sana kutokana na kuwa kila mmoja
atakuwa anavuna kahawa yenye ubora.
Ameeleza kuwa kanuni za
kilimo bora anazopaswa kuzingatia ni kuzingatia muda wa kupanda mche wa kahawa,
hadi kufikia wakati wa kuvuna kahawa kwa kufuata taratibu zote zinazoelekezwa.
Pia Kanjagaile ameeleza
kuwa sasa msimu wa kuanza kuvuna kahawa
mwaka huu umekaribia wakulima hawana budi kuhakikisha wanavuna kahawa
iliyokomaa na kuianika sehemu nzuri kama ambavyo wamekuwa wanaelekezwa na
wataalamu wa kilimo ili kupata bei nzuri ya zao hilo.


Post a Comment