Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: KUTUMIA MUDA MWINGI KUMTUMIKIA MUNGU NI FAIDA KWA MAISHA YA HAPA DUNIAN
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Wakristo wametakiwa kumtegemea Mwenyezi Mungu katika maisha yao ya hapa Ulimwengu kwani Mungu pekee ndiye anaweza kuwaepusha na majaribu ya...
Wakristo wametakiwa kumtegemea Mwenyezi Mungu katika maisha yao ya hapa Ulimwengu kwani Mungu pekee ndiye anaweza kuwaepusha na majaribu ya shetani.

Ushauri huo umetolewa na mwinjilisti Joyce Simoni katika ibada takatifu ya Kanisa la Pentekoste Tanzania bonde la upako wa Goshen Kayanga.

Mwinjilist Joyce amesema kuwa wakristo wote wanastahili kumuomba mwenyezi Mungu katika roho na kweli ili washinde mitego ya shetani na roho chafu zenye kuangamiza imani yao.

Ametaja baadhi baadhi ya dhambi ambazo zinaweza kuwatenga na Mungu kuwa ni pamoja na chuki binafi,matusi,udhalimu,wizi,ufisadi,na mambo mengine ambayo yako kinyume na mapenzi ya Mungu.


Mwinjilist Joyce amewambia waumini kuwa imani chanzo chake ni kusikia kwa hiyo  wampe Mungu nafasi katika maisha yao na wasibaki na huzuni wala manunguniko katika mioyo yao kwani Mungu yuko pamoja nao.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top