Halmshauri ya wilaya ya Karagwe kupitia idara ya kilimo
wametoa tahadhari kwa wakulima wilayani humu wanaojihusisha na vitendo vya
uvunaji wa kahawa mbichi na uuzaji wa kahawa za magendo (Ubutura) vitendo
vinavyosababisha kukosa kahawa zenye ubora.
Afisa kilimo Mkaguzi wa Kahawa
wilaya ya Karagwe Cleophace Kanjagaire amesema kuwa kwa sasa kuna baadhi ya
maeneo wakulima wameanza kuvuna kahawa mbichi na kuuza magendo jambo ambalo
amelitaja kuwa ni kunyume na sheria na atakayekamwa anafanya hivyo atachukuliwa
hatua za kisheria ikiwemo kunyanganywa kahawa hizo na kulipa faini.
Kanjagaire amesema kuwa tayari watendaji wameshapewa
barua za kuangalia suala laukaguzi na
udhibiti wa ubora wa kahawa katika maeneo yao na hilo linatakiwa
kuzingatia na kuhakikisha hakuna mkulima anayevuna kahawa mbichi.
Ameongeza kuwa hakuna mkulima anayekatazwa kuvuna kahawa
lakini anatakiwa avune zile zilizoiva kwani uvunaji wa kahawa mbichi unaharibu
ubora wa kahawa na sheria inakataza vitendo hivyo.
Post a Comment