Benki ya CRDB tawi la Karagwe imetoa zawadi ya mashine ya
kudurufu (Photocopy mashine) yenye thamani
ya shilingi million tatu kwa shule ya msingi Kayanga ikiwa
ni sehemu ya
maadhimisho ya mtoto
Afrika ambayo hufanyika Juni 16 kila
mwaka Afrika nzima.
Zawadi hiyo imetolewa leo na uongozi wa CRDB tawi la
Karagwe kwa lengo la kuchochea ufaulu mzuri
kwa wanafunzi wa shule hiyo na hatimae waweza kufikia malengo yao.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Karagwe Jeremiah Msemo amesema zawadi hiyo imetolewa na
benki yake kwa shule hiyo,ni motisha kwa walimu na
wanafunzi hao ili
waweze kuongeza ufaulu kwenye
masomo yao.
Msemo amesema anaamini kupitia zawadi hiyo iliyotolewa
itasaidia wanafunzi kufikia malengo yao na kusema kuwa ni
jukumu la wazazi na walezi kushirikiana
na walimu ili kuinua ufaulu wa wanafunzi hao.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kayanga
mwalimu Osward Marcel amesema kutokana
na zawadi hiyo iliyotolewa shuleni hapo anaamini ufaulu wa wanafunzi hao
utaongezeka kutoka asilimia 91 na kufikia asilimia 100.
Katika hatua nyingine benki ya Crdb tawi la Karagwe
imesherekea siku ya mtoto wa Afrika na watoto mbali mbali kutoka maeneo tofauti
wenye akaunti na wasio na akaunti ya watoto iitwayo Junior Jumbo katika benki
hiyo.
Kupitia maadhimisho hayo Meneja wa Benki ya Crdb tawi la
Karagwe Jeremia Msemo amewataka wazazi na walezi wa watoto wote kuwafungulia
akaunti watoto wao katika benki ya Crdb kwa ajili ya kuwajengea tabia ya kutunza
akiba wakiwa wadogo na baadae kuwawezesha kufikia malengo yao mbali mbali ya
baadae.
Post a Comment