Jeshi
la zimamoto na uokoaji mkoani KAGERA limeokoa mwili wa mvuvi mmoja
aliyekutwa amekufa huku mwili huo ukielea juu ya maji katika Bandari ya manispaa ya Bukoba.
THOMAS EMMANUEL mkaguzi msaidizi wa zimamoto mkoani KAGERA amesema kuwa tukio hilo la uokozi wa mwili huo limefanyika ikiwa siku chache zilizopita jeshi hilo limeokoa miili ya watu wengine watatu katika kata ya Bakoba na kufikisha jumla ya watu nne ambao wamekufa maji kwakipindi cha siku nne.
EMMANUEL amesema kuwa matukio haya yanatokea kutokana na upepo mkali uliopo katika ziwa Victoria ambapo amebainisha kuwa wakati matukio ya uokozi yakiendelea jeshi la polisi halikufika katika eneo la tukio na baada ya kuupeleka mwili huo katika kituo cha polisi umekataliwa na kupelekwa katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Kagera.
Shuhuda wa tukio hilo TEMI KALIMBE mkazi wa Kastamu amesema kuwa mtu huyo ambae mwili wake umeokolewa ukiwa unaelea juu ya maji na alikuwa anajishughulisha na uvuvi.
Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata Bakoba MAICO MGOE amesema kuwa kila mtu anatakiwa kuchukua tahadhari pale anapofanya kazi mwambao wa ziwa vicktoria ili kuepuka vifo visivyo vya lazima.
Hata hivyo baada ya uokozi huo mkaguzi msaidizi wa zimamoto na uokoaji mkoa wa KAGERA ,amewatahadhalisha wananchi wote wanaofanya shughuli za uvuvi ndani ya ziwa Victoria, kuhakikisha wanakuwa na vifaa vya uokozi hasa kwa kipindi hiki ambapo kuna upepo mkali
Post a Comment