Wananchi wa kijiji cha
Katwe Kata ya Kituntu Wilayani Karagwe Mkoa wa Kagera wametakiwa
kuchangia michango ya madawati haraka iwezekananvyo kuanzi kesho juni15 mwaka huu waatakaokuwa
hawajachangia mchango huo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Wito huo umetolewa leo na Afisa
mtendaji wa Kijiji cha Katwe Revitas Chuma
wakati akiongea na KARAGWE FORUM kuhusu wananchi katika kijiji hcho
kuchangia michango wa madawati.
Chuma amesema uchangiaji wa
madawati ni jukumu la kila mwananchi ili kuhakikisha wanafunzi wanakuwa na
madawati ya kutosha na kusema kuwa atakayekiuka agizo hilo sheria dhidi yake
zitachukuliwa.
Amesema muda uliotolewa kwa
wananchi hao kuchangia kwa hiari umetosha hivyo watakaoshindwa kutimiza wajibu
wao watawajibishwa ili kuhakikisha nao wanashiriki zoezi hili.
Post a Comment