Jumla ya madawati 40
kati ya 94 yanayohitajika yametengenezwa katika kijiji cha Rwabigaga kata ya
Kamuli Wilayani Kyerwa pamoja na kuwepo
kusuasua kwa wananchi kuchangia na changamoto ya kuchelewa kutolewa kwa fedha
ya mfuko wa Halmashauri.
Chombo hiki
kimezungumza na mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Rwabigaga Datus Rugemalila
Baziwani ambapo amethibitisha kukamilika
kwa utengenezaji wa madawati hayo kiasi cha fedha kilichokusanywa na matumizi
yake pia akabainisha changamoto wanazokabiliana nazo katika utekelezaji.
Aidha amesema wadau wa
maendeleo wamejitolea vifaa mbalimbali
vya kutengeneza madawati lakini wanakabiliwa na changamoto wa uhaba wa mafundi.
Vile vile amesema kupungua kwa kasi ya kukamilika kwa mradi wa
kutengeneza madawati inasabaishwa na
kucheleweshwa kwa fedha zilizotolewa na halmashauri ambapo kazi iliyofanyika
hadi hivi sasa inahitaji kukaguliwa ili fdha hizo ziweze kuhidhinishwa kutolewa
jambo ambalo hadi sasa halijafanyika.
Pamoja na changmoto
hizo Baziwani amekieleza chombo hiki kuwa
kazi inaendelea na kufikia mwishoni mwa mwezi huu kijiji hicho kitakuwa
kimekamilisha utengenezaji wa madawati waliyopangiwa.
Post a Comment