Mbunge wa jimbo la Kyerwa Innocent
Seba Bilakwate ameombwa
kufika nyumbani kwa
Begumisa Isaack kwa ajili ya
kuonesha utu wa kuwajali
watu wenye ualibino
kwasababu ya mateso
na manyanyaso wanayoyapata
kwenye jamii.
Wito huo
umetolewa leo na mkurugenzi wa
shirika la UNDER
THE SAME SUN
Vicky Ntetema wakati akiongea
na wananchi kupitia
Redio Fadeco kufuatia kuwepo
kitendo cha kufukua kaburi
la mtoto Magufuli
Begumisa wa kata
ya Businde wilayani
Kyerwa.
Amesema Mbunge
wa jimbo la
Kyerwa kuonesha kuwa anawajibika kwa
wananchi wake ni
vema akafika kwenye
eneo la tukio
kumjulia hali jambo
litakaloongeza imani kwa
watu wenye ualibino.
Ntetema amesema
kuwa utashi wa kisiasa kwa
nchi ya Tanzania
haupo kutokana na
wabunge kutoonesha dalili
zozote za kuhamasisha
kutunga walau sheria
maalumu ya kuwathibiti watu wanaojihusisha na
vitendo vya kinyama
dhidi ya watu
wenye ualibino.
Kwa upande
wake Afisa ustawi wa jamii
Ester Rwela katika shirika
la UNDER THE
SAME SUN amesema jamii
inabidi kuchukua jukumu
la kuhakikisha dunia
inakuwa mahali salama
kwa watu wenye
ualibino kwa kutoa
ushirikiano na kuonesha
upendo kwa kuwachangia
baadhi ya gharama
za afya ya mwili
wao.
Hata hivyo
VICKY NTETEMA amesema
jukumu la ulinzi dhidi
ya watu wenye
ualibino ni la
kila mmoja kwenye
jamii na kuwataka
wazazi wenye watoto
wenye ualibino
kutowatelekeza kwenye kambi
na badala yake
wawatembelee na serikali
inafanya utaratibu wa
kuwaweka kwenye shule
mchanganyiko ili kuwaondolea
imani ya kukaa
pekee yao.
Post a Comment