Serikali imeendelea
kusisitiiza kuwa haitasita kuwachukulia
hatua kwa kuwanyanganya vitalu
wawekezaji watakaobainika kukiuka
kufuata na masharti ya kampuni ya
ranchi za (NARCO ) waliopoewa wakati wa kumilikishwa vitalu hivyo
Rai hiyo imetolewa na kaimu
meneja Mkuu wa kampuni ya Lanchi za
Taifa (NARCO) Bwire Kafumu Mwijarubi wakati akiongea juu ya mienendo ya
wawekezaji waliomilikishwa na vitalu vya mashamba ya Lanchi yaliyoko ndani ya ranchi ya Missenyi iliyoko Wilayani humo Mkoani Kagera
Bwire amesema wakati
serikali inafikia uamuzi wa kutoa fursa
kwa wawekezaji kuwekeza kwenye vitalu
vya Lanchi za Taifa ililenga kuwainua wafugaji wa Ndani kuwekeza katika ufugaji wa kisasa wa ng’ombe bora kwa kupata utaalamu kutoka katika mashamba ya Ranchi za Taifa ,hivyo
hakuna sababu za msingi mwekezaji kukiuka
masharti yaliyondani ya mikataba
Amebainisha kuwepo maeneo
mengi yaliyovamiwa na wafugaji kutoka
Nchi jirani ,huku baadhi ya wafugaji haram wakidaiwa kuingizwa nchini na wananchi waliojirani na Lanchi, na wengine wanadaiwa kuingizwa kwenye vitalu vya
wawekezaji kwa kukubaliana na wawekezaji
hao jambo ambalo ni kinyume cha taratibu
zilizokubaliwa huku akisema
watakaobainika ni kunyanganywa vitalu hivyo mara moja.
Amesema kwa madhumuni ya
Ranchi za Taifa kama yalivyomasharti
mengine ya Umma ni kujiendesha
kibiashara hivyo mpango mkakati wa NARCO
ni kuhakikisha mashamba ya ranchi
yanaboreshwa na kuendelea kutoa huduama kama mashamba darasa kwa
wafugaji,wataalam mbalimbali pamoja na wanavyuo mbalimbali vilivyondani na nje
ya Nchi.
Ameongeza kuwa mashamba haya
ni magala ya mifugo ya Taifa ,hivyo NARCO itaendelea kuboresha mashamba yake
kwa kushirikiana na wawekezaji wa ndani na nje pmaoja na kufuatilia mashamba na
vitalu vilivyowekezwa kwa wawekezaji wakubwa kutoka nje ya nchi na wawekezaji wa ndani
lengo likiwa ni kuhakikisha kunazalishwa ngombe bora hapa Nchini.
Naye meneja wa Lanchi ya
Missenyi Martine Radslausi amesema kuwa
moja ya changamoto kubwa inayosababishwa uvamizi wa mifugo kutoka Nchi jirani ni vifo
vingi vya mifugo ya ranchi kutokana na
kushambuliwa na magonjwa ambayo huingizwa na Ng’ombe wageni.
Post a Comment