Idara ya uhamiaji
mkoani Kagera imewakamata wahamiaji haramu 58 kwa kosa la kuingia nchini
kinyume cha sheria katika kipindi cha siku 13 za mwezi Juni mwaka huu.
Mkuu wa uhamiaji mkoa wa Kagera, ABDALLAH TOWO amesema kuwa, kati ya wahamiaji hao, raia wa
Burundi ni 42, Rwanda 12, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni wawili na
Uganda wawili.
Aidha katika hatua nyingine TOWO amesema kuwa, idara hiyo ipo katika
mchakato wa kuwarejesha nchini mwao raia wanne wa Ethiopia
waliomaliza kifungo chao cha mwaka mmoja, baada ya kuhukumiwa kifungo
hicho kutoka na kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria.
Hata hivyo amewataka wageni kufuata sheria za nchini huku akiwataka wakazi wa
mkoa wa KAGERA kuwaulizia uraia wageni wanapotoka katika nchi zao ili
kuwajua vizuri.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment