Wito huo umetolewa na Fabian Tibandebage wakati akiongea na waandishi wa habari wanaozungukia vituo mbalimbali vinavyotumika kuhawilisisha fedha wilayani hapa amesema kutokana na baadhi ya walengwa wa TASAF wanaopokea ruzuku ya masharti wasipofanya hivyo husababisha kupokea pesa pungufu na kusababisha kuanza kulalamika.
Ametaja masharti
ya ruzuku hiyo
kuwa ni kupeleka
mtoto Kliniki na shuleni
hivyo wasipojaziwa famu
hizo na wahusika
husababisha kukatwa pesa
hiyo ili aweze
kutimiza masharti hiyo.
Kwa upande
wake afisa mtendaji
wa kijiji cha
Kanywamagana kata ya
Nyakakika Henry Hezironi amesema
changamoto kubwa inayowakabili
kwa sasa katika
kijiji hicho kwenye
zoezi la kuhawilisha
fedha hizo ni kuwepo
wahamiaji haramu ambapo
hivi sasa wamebuni
njia mpya ya
kujiingiza kwenye mpango huo
kwa ktumia majina
ya wenyeji ambayo
ni ngumu kuwatambua.
Hezironi amebainisha
walengwa wa mpango
huo walioondolewa kwenye
kijiji hicho cha
Kanywamagana kwa kukosa
sifa za kuendelea
kupokea pesa hiyo.
Aidha Afisa
Maendeleo ya jamii
kata ya Kibondo
Gloria Joackimu amesema
elimu zaidi inahitajika
kuendelea kutolewa kwa
njia mbalimbali kwa
walengwa kuhakikisha wanatambua
umuhimu wa kutimiza
masharti ya ruzuku
kuepusha usumbufu wa
kukatwa fedha.
Hata hivyo
mafanikio ya mpango
wa kunusuru kaya
maskini yamebainishwa kuwa
yamepatikana kwa walengwa kuongeza
matumizi na wengine
kuwa na miradi
ya kuwaongezea kipato.
Post a Comment