Jumla ya walengwa 120 kati
ya walengwa 6156 waliokuwa wakipokea
ruzuku inayotolewa na serikali kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini Nchini (TASAF III) Wameondolewa kwenye mpango
kutokana na kukosa sifa huku wengine
wakibainika kuwa ni wahamiaji haramu
Kwa mjibu wa Mratibu wa
Tasaf Wilayani Misseny Joramu Karugaba ,idadi ya walengwa hao imebainika baada ya zoezi la uhakiki upya wa walengwa hao ambao wengi wao waliingizwa
kwenye mpango kutokana na kupitishwa kwenye mikutano yao ya vijiji.
Kalugaba amebainisha kuwa
walengwa hao wameibuliwa kutoka ndani ya vijiji 50 vilivyopo kwenye mpango wa
TASAF na jumla ya wahamiaji 26 waliokuwa ndani ya mpango wa kupokea
ruzuku hiyo walipatikana katika kata ya kakunyu ,huku
walengwa wengine wakiondolewa kutokana na sababu za vifo na wengine wakidaiwa kuwa wajumbe wa serikali za vijiji kunufaika na ruzuku hizo.
Amesema kutokana na walengwa
hao kuondolewa kwenye mpango,kiasi cha
shilingi million 209,768,000 zitatolewa
kwa ajili ya ruzuku kwa malipo ya
mwezi Mei na Jun,fedha zitakazowanu
faisha walengwa 6156 katika Wilaya hiyo.
Kwa upande wake Yohanesi
Nchimbi ambaye ni Afsa Mshauri na ufuatiliaji wa mpango wa TASAF
III Wilyani Misseny walengwa hao
walibainika tiyari wakiwa wameingizwa kwenye
mfumo wa kupokea ruzuku hizo,ambapo tiyari walikuwa
wameishapokea fedha ya ruzuku ya awamu ya Kwanza,pili na tatu kabla ya utaratibu wa kuwaondoa
na malipo ya awamu ya nne hadi sasa hawakupokea ruzuku hiyo.
Hata hivyo Nchimbi amesema
kuwa ,taratibu za kubainishwa mlengwa
mwenye sifa na vigezo vya
kuingizwa kwenye mpango wa kupokea ruzuku uko mikononi mwa mkutano wa kijiji,hivyo kuwashauri
wananchi kujenga utamaduni wa kuhudhulia mikutano inayoitishwa kwenye vijiji vyao ili kuweza
kupitishwa mipango inayolenga
kuboresha maisha yao na kuwaletea maendeleo kwa ujumla.
Post a Comment