Wananchi
wanaotumia ziwa Victoria katika shughuli mbalimbali ikiwemo uvuvi
wametakiwa kuchukua tahadhari katika kipindi hiki ambapo ziwa hilo
limechafuka kwa kuwa na upepo mkali.
Kamanda wa polisi mkoani KAGERA AUGUSTINE OLLOMI amesema hayo baada ya
kuwepo kwa taarifa za matukio ya watu kufa maji katika ziwa hilo ambayo
yanasababishwa na upepo.
Amesema kuwa,kumetokea matukio mawili tangu kuanza kwa mwezi june,ambapo katika
tukio la kwanza watu watatu walifariki huku tukio la pili likimhusisha
mtu mmoja aliyekutwa mwili wake ukielea juu ya maji siku mbili baada ya kuaga
nyumbani kuwa anakwenda kuvua samaki.
Hata hivyo amewataka wavuvi kutumia vifaa vya kujiokolea kama lifejacket pindi
kunapotokea ajali ya mitumbwi yao kupigwa dhoruba au kuzama.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment