Wazazi,walezi na jamii wametakiwa kuacha kutoa adhabu kali
zinazowaumiza watoto na baadala yake wawaelekeze katika maadili yanayositahili .
Wito huo umetolewa leo na
Wanachama wa Kikundi cha Pamoja Tunaweza ambacho kimeundwa
kupitia Redio Fadeco kilichopo kata ya Nyaishozi wilayani Karagwe chenye lengo la kutokomeza
vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ambavyo vinafanywa na baadhi ya wazazi,
walezi pamoja na jamii.
Naye mhudumu wa afya wa kijiji cha Nyakayanja wilayani Karagwe
Amoni Matayo amesema Mtoto anapofanya kosa
nivyema kumkanya na siyo kumpatia adhabu zinazomuumiza .
Pia Janeth Baraka mkazi wa Akajiji amesema kuwa mtoto
ambaye yupo chini ya umri wa miaka 18 anahitaji malezi kutoka wazazi na akifanya
kosa unatakiwa kumuhoji kulingana na kosa alilofanya kabla ya kumpatia adhabu .
Katibu wa kikundi cha pamoja tunaweza Helina Bisimeki
amesema amewiwa kujiunga na kikundi hicho ili kuwa balozi wa watoto na wanawake
katika kutoa elimu baada ya kuona watoto wanapata manyanyaso mbalimbali kwenye
jamii.
Ameiasa jamii
kutoa ushirikiano kwa kikundi hicho ili kuhakikisha wanatokomeza vitendo vya
ukatili dhidi ya watoto.
Post a Comment