MAFANIKIO
KIMAISHA HAYAKAI KWENYE VYETI:-
Na
Albert Nyaluke Sanga
Nikiwa
mwaka wa kwanza Chuo Kikuu Cha Tumaini- Iringa (sasa wanakiita University Of
Iringa); nilikutana na jamaa mmoja aliyekuwa ndio kwanza ametua nchini baada ya
kumaliza shahada yake ya kwanza katika moja ya vyuo vikuu nchi ya jirani hapo
kwa Museveni.
Jamaa
huyu akaniambia kauli ya ajabu sana, akasema, "Kwa nini umeenda kusoma
chuo hicho?(akimaanisha Tumaini). Wenye akili wako UDSM(Akimaanisha chuo kikuu
cha Dar es Salaam, maarufu kama Mlimani), huko Tumaini umeingia choo cha kike,
utachelewa sana kuajiriwa".
Nikamwangalia weeee, (nikamuhurumia na kumdharau ndani kwa ndani) halafu
nikamjibu kwa hasira; "Brother, wenye akili ni wale wenye hela za maana;
wanaweza kuwa wamesoma huko UDSM ama chuo chochote na wanaweza kuwa hawakusoma
kabisa!. Kujidhania una akili za kufaulia mitihani halafu usiwe na hela za
maana(au angalau za kutosha) huo ni ujuha."
Akiwa
bado anashangaa-shangaa nilichomwambia, nikamuongezea; "Kwanza
wanaohangaika na CV za mavyuo ni wale wanaotaka kuwavutia wenye akili (waajiri)
ili wawaelekeze cha kufanya(yaani wawaajiri). Mtu mwenye maono ya kujiajiri
hahangaiki na CV za mavyuo bali anaangalia maarifa ya kumsaidia na kimsingi
anaweza hata asiende shule bali akayapata maarifa hata mtaani tu".
Akaniuliza, "Unamaanisha nini?"
Nikamjibu
swali lake:- "Brother umesoma chuo Kikubwa lakini bado una akili za
kikoloni zinazowaza kuwa hakuna maisha ya maana mpaka uajiriwe. Kusoma ni jambo
zuri na kuajiriwa sio jambo baya lakini usikariri kuwa hakuna maisha pasipo
kuajiriwa; na usifikiri kila anaefika chuo kikuu anawaza kuajiriwa tu”. Yule
brother alipaniki nusura anizabe makofi, nikaamua kuondoka "fasta" na
kiukweli nilimchanganya na kumuudhi sana. Unajua ni nini? Ngoja nikupe pointi
tatu fasta fasta:-
1.
Siku hizi mafanikio kimaisha hayamo katika CV ya chuo ulichosoma na kamwe
hutatajirika (au angalau kuwa na pesa za maana) kwa kutegemea mshahara
pekee". Ikiwa imepita miaka saba sasa, sijajua hali ya kiuchumi na
kimaisha ya yule brother; lakini ikiwa hajabadilisha ile "mentality"
nina uhakika atakuwa "ni mbangaizaji tu" kiuchumi na kimaisha kwa
ujumla licha ya kuwa anamiliki cheti cha digrii kutoka nchi ya ng'ambo!
2.
Hili ni tatizo lililopo miongoni mwa wasomi wetu wengi, wanachanganya nafasi ya
maarifa na vyeti. Kwao kumiliki cheti cha ngazi fulani kutoka chuo fulani, ni
muhimu zaidi kuliko ubora wa maarifa anayokuwa nayo kichwani. Vijana wanatakiwa
kutambua kuwa muundo wa soko la ajira umebadilika sana, soko la ajira linazingatia
uwezo wa muhitimu kushinda jina la shule ama chuo alichosoma muhitimu.
3.
Nimekuwa nikiwaeleza wasomi kwamba, “Ukishamaliza kazi ngumu ya kujifunza
"profeshino" yako; iwe ni ualimu, udaktari, uanasheria, uinjinia,
n.k; basi ni vema usisahau pia kujifunza jinsi ya kutafuta hela. Kupata hela za
kawaida kupitia mshahara utazipata tu; kwa; hiyo "profeshino", ila
kwa "case" ya kuwa na hela za kutosha itakulazimu ujifunze mtaala
mwingine mbali na hiyo "profeshino". Kwa sababu "profeshino"
bila kuwa na hela za kutosha ni mzigo” #SmartMind
Post a Comment