Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: SAFU YA WATENDAJI WALIOTEULIWA NA RAIS MAGUFULI KWA MKOA WA KAGERA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Mkoa   wa   Kagera   umepata   watendaji   wapya   kwa   nafasi   za   mkuu   wa   mkoa ,wilaya,   makatibu   tawala   na   wakurugenzi ...

Mkoa  wa  Kagera  umepata  watendaji  wapya  kwa  nafasi  za  mkuu  wa  mkoa ,wilaya,  makatibu  tawala  na  wakurugenzi wa  halmashauri  za  wilaya   na  baadhi  waliokuwepo  mkoani  hapa  wakihamishwa vituo  vyao  vya  kazi  na  wengine   wakiachwa  katika   uteuzi  wa Rais  wa  Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania  DK  John   Pombe.

Kwenye  nafasi  ya  mkuu  wa  mkoa  wa  Kager aliteuliwa  Meja  Jenerali  Mstaafu  Salum Mustapha  Kijuu  kuchukua  nafasi  ya  John  Mongella  ambaye  katika  uteuzi  wa  nafasi  hiyo  alihamishiwa  mkoani   Mwanza.

Katika  nafasi  za  wakuu  wa  wilaya  walioteuliwa  kuongoza  wilaya   saba  za  mkoa  wa Kagera   wilaya  ya  Karagwe  ni Geofrey Muheluka Ayoub ,wilaya  ya  Kyerwa aliyeteuliwa   ni  Kanali Mstaafu  Shabani  Ilangu Lissu, Biharamulo  aliyeteuliwa  ni Saada Abraham Mallunde,Missenyi   ni  Luten Kanali Denis F.Mwila  , wilaya  ya  Ngara  ni Luten Kanali Michael  M. Mtenjele  na Bukoba  ni  Deodatus  Lucas  Kinawiro.

Rais  Magufuli  pia  katika  nafasi  za  makatibu  tawala  amewateua  Gread  Clement Ndyamukama kwa katibu  tawala  wilaya  ya  Bukoba,Biharamulo   ni  Joel  Mwakabibi ,Ngara Josephat V. Tibaijuka ,Muleba ni Mwakasyege Benjamin  Richard ,Missenyi  Godrey  Msongure  Kasekenya,Karagwe  katibu  tawala  aliyeteuliwa  ni  Weja  Lutobola Ng’olo na wilaya  ya  Kyerwa  ni  Haji Yusuph   Godigodi.

Pia  Rais  John  Magufuli amekamilisha  safu  hiyo  kwa  mkoa  wa  Kagera  kwa  kuwateua  wakurugenzi  watendaji  wa  halmashauri  za  wilaya  za  mkoa  huu  ambao  ni Biharamulo Wende Israel Ng’ahala, Bukoba  Abdulaaziz Jaad Hussein, Bukoba Manispaa,  Makonda Kelvin Stephen,  Karagwe, Godwin Moses Kitonka,  Kyerwa Shedrack M. Mhagama, Missenyi Limbe Berbad Maurice,  Muleba ,Emmanuel Shelembi Luponya  na  Ngara  ni  Aidan John Bahama


Katika  safu  ya  serikali  ya  awamu  ya  Tano ya  Rais  Magufuli walioteuliwa kutoka mkoa  wa Kagera ni  Professa  Faustin Kamzora kuwa  katibu  mkuu  wa  wizara  ya  mawasiliano,Charles  Mwijage kuwa  waziri  wa  viwanda  na  uwekezaji, Audax  Christian Rukonge ambaye aliwania Ubunge wa jimbo la Karagwe aliishia ngazi  ya kura za maoni ndani ya CCM ameteuliwa  kuwa  mkurugenzi  mtendaji  halmashauri  ya  Ulanga  mkoani  Morogoro na  Jordan Rugimbana   kuwa  mkuu  wa mkoa  wa  Dodoma.

Wengine ni    Ruth  Blasio Msafiri ambaye  aliteuliwa mkuwa mkuu  wa  wilaya  ya Njombe  mkoani Njombe na Sumpter  Nshunju Mshama ambaye  ameteuliwa kuwa  mkuu  wa  wilaya  ya  Kibaha  mkoani Pwani.

Hata hivyo Dary  Ibrahimu  Rwegasira aliyekuwa mkuu wa  wilaya ya  Biharamulo , Luteni  Mstaafu  Ole  Lenga wa Kyerwa ,Honoratha  Kitanda wa Ngara ,Jackson Msome wa Bukoba  na Fransis Isaack   wa  Muleba  wameachwa  kwenye  uteuzi  wa  serikali  ya  awamu  ya tano.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top