Watumishi wa
serikali waliopewa jukumu la
kujaza taarifa za watoto
walio katika mpango wa
kunusuru kaya maskini
wa TASAF III kuhakikisha wanazijaza
kikamilifu na wale
ambao wanakataa kuzijaza kwa
kisingizio cha kutaka
kulipwa posho ya
kazi hiyo wametakiwa
kuripotiwa mara moja
ili waweze kuchukuliwa hatua
za kinidhamu dhidi
yao.
Kauli hiyo
imetolewa na mwenyekiti
wa halmashauri ya
wilaya ya Karagwe
Wallesi Mashanda wakati
akitoa elimu na
hotuba kwa walengwa
wa kunusuru Kaya
maskini wa kijiji
cha Kanoni Kata
ya Kanoni ikiwa
ni mwendelezo wa
kamati ya fedha, mipango na
uchumi inayoendelea ya
kutembelea walengwa na
kuwapa elimu ya
matumizi sahihi ya ruzuku wanayoipokea.
Amesema katika
taarifa fupi iliyosomwa
na mtendaji wa
kijiji imebainisha kuwepo
baadhi ya watumishi
wa serikali ambao wameajiriwa
kwa lengo la
kutoa huduma kwa
wananchi lakini wanashindwa kufanya hivyo
wakihitaji kulipwa au
kusababisha mazingira ya
kupewa rushwa hivyo
hawatamvumilia mtu huyo.
Mashanda amewataka
walengwa wa mpango
wa TASAF III kutumia
ruzuku wanayoipokea kwa
malengo yaliyokusudiwa na watakaoenda kinyume
na malengo hayo
kwa kunywa pombe
na kufanyia mambo
ambayo yanachangia kurudisha
maendeleo nyuma hawatasita
kumwondoa mara moja
kwenye mpango.
Amewataka pia
kuhakikisha wanaweka mkakati
wa utunzaji mazingira
kwa kupanda miti
rafiki ya kutunza
uoto wa asili
pia watumie fursa
hiyo kama njia
ya kujikwamua kiuchumi
kwani wakipanda miti
ya matunda wataweza kuuza na
kujiingizia fedha.
Naye diwani
wa Nyakahanga Charles
Bechumila ambaye ni
mwenyekiti wa kamati
ya kudumu ya
afya,elimu na maji
amewataka walengwa wa
mpango huo kujiunga
na mfuko wa
jamii wa CHF
ili waweze kupatiwa
matibabu ya bure kwa
mwaka mzima kwa
Kaya yenye watu
sita wanachangia shilingi
elfu kumi na
Tano tu.
Hata hivyo
walengwa waliotembelewa kwenye
makazi yao wameelezea
pesa hizo zilivyowasaidia kubadilisha
maisha yao na sasa
walivyo kutokana na
kupokea ruzuku hiyo.
Post a Comment