Wanafunzi wametakiwa kushiriki michezo mbalimbali wanapokuwa shuleni kwani kufanya hivyo kunawasaidia wao kuwa na wigo mpana wa kujiajiri nje na kutegemea elimu ya darasani tu.
Wito huo umetolewa
na Miss Baramba
Sekondari kwa mwaka
2016 Jovither Dominick wakati
akiongea na Redio
Fadeco mara baada
ya kutangazwa mshindi
wa taji hilo
kwa mwaka huu katika
tamasha la utamaduni
shuleni hapo ambalo
hufanyika kila mwaka
na kuhusisha michezo
mbalimbali ya kitamaduni.
Amesema kuwa kupitia
michezo fani mbalimbali
ambazo zimejificha kwa
wanafunzi ni nyingi
hivyo zinahitajika kuwa
tayari kushiriki pale
wanapopata fursa ya
kuelekezwa au kuhimizwa
na walimu wao.
Jovither
Dominick amesema yeye
kuwa Miss Baramba
Sekondari inawezekana ikwa
mwanzo wa kufungua
milango ya kujihusisha na fani
hiyo huku akisema
kuwa anaweza kujiongezea kipato
kwa kutoa ushauri
hata kama atakuwa
ameajiriwa kwa fani
nyingine tafauti na
urembo
Katika siku hiyo ya siku ya utamaduni maarufu kama CULTURAL DAY kulekuwepo na mashindano ya kumpata mshindi wa jumla ambao walikuwa wakishindana kwenye vipengele vya ngoma, kuimba, maingizo ambao makundi yalikuwa matatu ambayo yamepewa majina ya Ana Tibaijuka,Ana Makinda na Asha rose Migiro hiyo hutumika kutambulisha wanawake walioonyesha mfano wa kuongoza.
Mshindi wa jumla mwaka 2016 ni Ana Makinda House, Asha rose Migiro House ikishika nafasi ya pili na Ana Tibaijuka ikashika nafasi ya tatu ikiwa imeangushwa na baada ya kutangazwa washindi walikuwa na haya ya kusema.
Kwa upande
wao washiriki wa
shindano hilo la
miss Baramba Sekondari mwaka 2016
wameelezea kuridhika na
majaji wa shindano
hilo kuwa wameonesha
haki na wakasema
wanajivunia hatua waliofikia
huku wengine wakieleza
furaha yao.
Post a Comment