Wananchi wa
vijiji vya Muguruka
na Chamchuzi katika
kata ya Bweranyange
wilaya ya Karagwe
Mkoani Kagera wameiomba
serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa
Tanzania kuimarisha ulinzi
wa mpaka wa
Tanzania na nchi
ya Rwanda kwenye
mwalo wa Rukombe
na visiwa vilivyopo
kandokando ya mto
Kagera kutokana na
kuwepo vitendo vingi
vya uharifu.
Wakizungumza Jana
katika mkutano wa
hadhara uliofanyika katika
kijiji cha Muguruka
kata ya ya
Bweranyange ulioitishwa na
mkuu wa wilaya
ya Karagwe Godfrey
Mheluka ambao ulikuwa
na lengo la
kuwasikiliza wananchi kutoa
maoni na ushuhuda
wa vitendo vya
uharifu ambavyo vimeishapoteza maisha
ya Watanzania wengi.
Godoliva Gidioni
(43)alisema tatizo la
uharifu wa wananchi
kupigwa risasi hata
kama wapo kwenye
shughuli zao binafsi
ni mkubwa mno
na yeye alinusurika
kuwawa mwaka 2004 ambapo
alikuwa na mme
wake na mtoto katika
kisiwa cha Mubari
kilichopo mpakani walivamiwa
na watu wanaosadikiwa
ni askari wa
doria kwenye ziwa
la IHEMA ambalo lipo nchi
jirani ya Rwanda
“Kweli kwenye
kisa hicho nilikuwa
nimebeba mtoto walipiga
risasi ya kwanza
ikampata mme wangu
Gidion Balembengaro (30) akauwawa
mimi nilianza kukimbia
nikiwa na mtoto
mgongoni lakini nilipatwa
na risasi ambayo
ilimpiga mwanangu Rehema
Gidion miezi( 10) kipindi
hicho likapitiliza likanipata
mimi upande wa
mkono wa kulia
unaona hii alama
hivyo kushtuka nikakuta
mtoto wangu alishafariki”Alisema Godoliva
Dominick Benjamini
(41)alisema jambo la
ulinzi kwenye mwalo
wa Rukombe na
visiwa vya Mubari,Kisayo,Mto Kagera
na Kizinga ni
muhimu kuimarishwa hata
inavyotokea mtanzania anaenda
kwenye maeneo hayo
wakikutwa wanapigwa risasi
tena mchana alisema
watu hao wanakuwa
na bodi na
wanasadikika kuwa ni
askari wanaofanya doria
kwenye ziwa la
akiba la IHEMA lililopo Rwanda.
“Akimwonyesha mkuu
wa wilaya ya
Karagwe Godfrey Mheluka
kovu la risasi
alilopigwa kwenye bega
la mkono wa
Kulia na kwenye
kiganja cha mkono
wa kushoto alisema
alipigwa risasi hiyo
Agosti 16 mwaka 2013 na
alijiokoa kwa kijificha
kwenye tingatika lilipo
mpakani mwa Tanzania.
Kwa upande
wake Agustine Ngambeki (50)alisema yeye
alikamatwa Agosti 03 mwaka
huu wakati akiwa
eneo la mto
Kagera alipokuwa amehaidiana
na wafanyabiashara wa
Rwanda kumuuzia samaki
kwani eneo hilo
ni njia hivyo alikutwa
hapo akanusurika kupigwa
risasi baada ya
mmoja wa wanaofanya
doria kutompiga risasi
kwani eneo hilo
lilikuwa la Tanzania.
“Nilisurika kwasababu
kulikuwepo watanzania wengine
wanapita hivyo nikatoa
taarifa kwao na wao
kuzifikisha kwenye uongozi
wa serikali ya
kijiji ambapo na
wao walipeleka taarifa
kwenye ngazi ya wilaya nilipelekwa
hadi nchi Rwanda
nikawekwa gerezani lakini
tarehe 10 mwezi
huu mwenyekiti wa
kijiji alifika nchini
Rwanda na kuhaidiwa
wataniachia na Agosti 19
mwaka huu nilikabidhiwa
kwenye mpaka wa
Rusumo ndiyo nikalijea
hapa nashukuru uongozi
na wananchi “Alisema Ngambeki.
Akisoma taarifa
ya kata hiyo
Afisa Elimu kata
ya Bweranyange Godwin
Mbeikya kwa niaba
ya Mtendaji wa
Kata alibainisha kuwa
tangu mwaka 1972 watanzania
waliouwawa kwa kupigwa
risasi kwa vitendo
vya uharifu ni
56 ambapo kijiji
cha Muguruka ni 20
na Chamchuzi ni
watu 30 na wajane
ni 21 alibainisha kuwa
wanaiomba serikali ya
Tanzania kuweka kivuko
kwa ajili ya
kuimarisha ujirani mwema.
Alisema kuwa hao
ni baadhi ya
watanzania waliotoa taarifa
kwa serikali za
vijiji na kata
lakini wapo wengi
ambao hawatoi taarifa
hivyo kuna uwezekano wa
idadi kuongezeka kama zingelipotiwa
zote.
Mkuu wa
wilaya ya Karagwe
baada ya kusikiliza
shuhuda za wananchi
hao amepiga maruku
mwananchi yeyote yule
kuvua samaki kwenye
Ziwa IHEMA kwani
halipo nchi ya
Tanzania na kuwataka
kutoendeleza shuguli za
uvuvi kwenye Mto
Kagera na kutofanya shughuli katika
visiwa vya Mubari,Kizinga na
Kisayo mpaka pale
serikali itakapo kamilisha
utaratibu wa kupata
boti ya kuimalisha
ulinzi katika mpaka
huo.
Pia amuagiza
mkuu wa polisi
kwa kushirikiana na
wanajeshi wa jeshi
la wananchi wa
kambi ya Chamchuzi
na Kashanda kufanya
oporesheni ya kuwaondoa watu
wote waliovamia kwenye
visiwa vyote vilivyopo
Tanzania ambao inasadikika
siyo watanzania na
wanajihusisha na ulimaji
Bangi na mirungi na
ameongeza kuwa bado
kamati ya ulinzi
na usalama inakusanya
taarifa na baada
ya kukamilika zitapelekwa
kwa waziri wa
mambo ya ndani
kwa ajili ya
hatua zaidi za
kufanya mawasiliano na
serikali ya nchi
ya Rwanda hivyo
akawataka wananchi kuwa
watulivu.
Hata hivyo Agosti 11 mwaka huu
waziri wa mambo
ya ndani wa
Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mwigulu
Nchemba alitembelea mwalo
wa Katwe wilayani
Kyerwa baada ya
kuwepo taarifa za
watanzania wawili Emmanueli
Kahonda (35) Mkazi wa Kitwechenkula wilayani
Kyerwa na Mfuruki Felesian (40) mkazi wa Rubwera
wilaya ya Kyerwa
waliuwawa Agosti
8 mwaka huu.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchini
Mwigulu Nchemba aliiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kyerwa
kukutana na viongozi wa mialo ya Rubwera, Kanyika, Katwe na Ruko ili wapate taarifa
rasmi ya chanzo cha matukio hayo na kuipatia wizara ili waweze kutoa tamko
rasmi juu ya mauaji hayo ya wavuvi.
"Hali hii imenistua
sana,hatuwezi kuruhusu watanzania wenzetu wawe wanauwawa kikatili kiasi
hiki,nikipata taarifa rasmi nitafuatilia jambo hili hata kwa kuwasiliana na
wenzetu ili nijue kama ni msimamo wa serekali yao au ni uhalifu"alisema
Nchemba.
Post a Comment