Wananchi wilayani Karagwe mkoani Kagera wametakiwa
kuendelea kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli katika harakati zake za
kupambana ili kuleta maendeleo katika taifa la Tanzania akioonesha kufuata
nyayo za Baba wa Taifa hayati Mwalim Julius Kambarage Nyerere.
Wameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wakizungumzia
kumbukumbu ya kifo cha baba wa Taifa ambayo hufanyika kila oktoba 14 kila
mwaka.
Wamesema kuwa
Hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere anakumbukwa kwa mambo mengi
ikiwemo kutetea wanyonge,kukataa ukabila, udini, Rushwa pamoja na vitendo vya
unyanyasaji ambavyo katika uongozi wa awamu zilizopita vilikuwa vimeshamili na
kuifanya nchi ya Tanzania kuonekana ya wachache lakini kwa uongozi huu wa Rais
Magufuli unatia matumaini kwa walio wengi.
Aidha wameasa wananchi wenzao kufanya kazi kwa bidii
ikiwa ndiyo njia mojawapo ya kuendelea kumkumbuka baba wa Taifa kwani alikuwa
mchapakazi na mzalendo kwa taifa lake huku wakiowaomba viongozi wote wa serikai
kufuata nyayo hizo ili kuliweka taifa la Tanzania katika hali ya amani,utulivu
,haki na usawa.
Hata hivyo wananchi walioongea na kituo hiki wameeleza
kuwa na matumaini na uongozi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John
Pombe Magufuli wakisema kuwa kufikia 2020 atakuwa amerudisha nchi kama
ilivyokuwa wakati wa uongozi wa hayati Mwalimu Nyerere.
Itakumbukwa kuwa Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere alifariki dunia mnamo
tarehe 14 mwezi wa 10 mwaka 1999 ikiwa ni kumbuka ya miaka 17 tangu kifo chake.
Post a Comment