Baadhi ya
madreva katika mamlaka
ya mji mdogo
wa Kayanga wilayani Karagwe
wameelezea umuhimu wa Kampeini ya
ZUIA AJALI HAPA
kuwa inasaidia kutoa tahadhari kwa
watumiaji wote wa barabara.
Claudian Andrew ambaye ni dreva tax amesema kuwa ubovu wa vyombo vya usafiri ndio unaosababisha ajali na kuwataka madreva kuwa makini na vyombo vyao na kuepuka kuendesha magari wakiwa wamelewa ili kupunguza ajali zisizotarajiwa
Fadhili
Sued ambaye ni dreva wa gari la abiria (hiace) amesema kuwa wamenufaika na
wameelimika kupitia kauli hiyo.
Sued
amewashauri madreva wenzake wa magari ya
abiria kufuata kanuni na sheria za barabara na kuepuka mwendo kasi ili kulinda
uhai wa abiria.
Eliza Emmanuel ambaye ni abiria amesema kauli
hiyo ya HATUTAKI AJALI TUNATAKA kuishi imesaidia kupunguza ajali kwani madreva
wamepunguza mwendo kasi wawapo safarini na amewataka madreva kuendesha magari
kwa mwendo ulioruhusiwa na kufuata kanuni na sheria za barabara.
Ameishukuru
serikali kwa kufuatilia kwa makini
sheria kwa wanaokiuka masharti ya
barabarani. Pia amewataka madreva kupunguza mwendokasi ili kuokoa maisha ya watu.
Post a Comment