Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: NAIBU WAZIRI TAMISEMI SULEIMAN JAFFO AWATAKA WATUMISHI KUJITUMA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Naibu   Waziri   wa   ofisi   ya   Raisi   serikali   za    Mitaa   TAMISEMI   Suleiman   Jaffo   amewataka   watumishi     kufanya   ...

Naibu  Waziri  wa  ofisi  ya  Raisi  serikali  za   Mitaa  TAMISEMI  Suleiman  Jaffo  amewataka  watumishi    kufanya  kazi  kwa  bidii  na  kutambua  dhamana  waliokabidhiwa    na  serikali  ya  kuwatumikia  wananchi  katika  kuwaletea     maendeleo  na  atakayeshindwa  kufanya  hivyo awapeshe  wanaoweza kuwatumikia.

Ametoa  kauli  hiyo  leo  katika  Ukumbi  wa  kituo  rafiki  cha  Vijana  Maarufu  kama  Angaza  wakati  akiongea  na  watumishi  wa  halmashauri  wa  wilaya  ya  Karagwe  pamoja  na  wageni  waalikwa  waliohudhuria  mkutano  huo.

Naibu  waziri  amesema  kuna  baadhi  ya  watumishi  wa    hawaoneshi  thamani  yao  ya  uwepo  wao  katika  ofisi  za  umma  na  wanafanya  kazi  kwa  mazoea  hivyo  kuingiza  serikali  katika  hasara  kubwa  na  kusababisha   malalamiko  kutoka  kwa  wananchi  .
Jaffo  amemtaka  mkurugenzi  mtendaji  wa  halmashauri  ya  wilaya  ya  Karagwe  Godwin  Kitonka  kukaa  na  wakuu  wa  Idara  na  vitengo  kuweka  mkakati  wa  utendaji  kazi  kwa  mwaka  huu  wa  fedha  na ifikapo  mwezi  wa  saba  mwakani  kufanyike  tathimni  ya  makubaliano  hayo.


Aidha, amesema  hataki  kusikia  kuwa  Karagwe  kuna  tatizo  la  uhaba  wa dawa  kwenye  Zahanati  pamoja  na  vituo  vya  afya  kwani  tayari  serikali  imeishatoa  shilingi  million 420  kutoka  mfuko  wa  basket  fund  ambapo  asilimia 33  ya  fedha  hiyo lazima  itumike  kununua  madawa ili kusaidia  kuondoa  tatizo  la  dawa.

Amemtaka  mganga  mkuu   kuzingatia  muongozo  wa  wizara  kuhusu  matumizi  ya  fedha  hizo  kwani  kuna  baadhi  walikuwa  wanaitumia  kama  njia  ya  kuendeshea  miradi  yao  binafsi.

Katika  hatua  nyingine  ameagiza  katibu  tawala  wa  mkoa  kusimamia  kwa  karibu  kuhusu  ujenzi  wa  wodi  mbili  za  kulaza  wagonjwa  katika  kituoa  cha  afya  Kayanga  kwani kikosi  cha  askari  wa  Jeshi  la  Wananchi  watafika  mwakani  kuanza  ujenzi  huo.

Kwa  upande  wake  mbunge  wa  jimbo  la  Karagwe  Innocent  Bashungwa  amemuomba  Naibu    Waziri  wa  TAMISEM  kusaidia  kutatua  changamoto  zinazoikabili  wilaya  ya  Karagwe  haswa  katika  sekta  ya  afya .

Naibu  Waziri  Jaffo akijibu  baadhi  ya  hoja  za  mbunge  amesema  ataendelea  kumpatia  ushirikiano   kwasababu  anajitihada  za  kuwatumikia  wananchi  waliomtuma  bungeni  hivyo  na  kuhaidi  kuwa  suala  la  ujenzi  wa  hospitali  ya  wilaya  atauandikia  ripoti  maalumu.

Hata  hivyo  amewataka  viongozi  wa  halmashsauri  nchini  kuwatumia  ipasavyo  maafisa  maendeleo ya  jamii    maana  wao  ni  mawakala  wa  mabadiliko  lakini  wamesahaurika   na  kubakia  kutumika  katika   matukio  maalumu  tu.










About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top