Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WATUMISHI WATATU KAGERA WATUMBULIWA NI KUHUSU PESA YA TETEMEKO
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
  Watumishi watatu wa manispaa ya Bukoba  mkoani  kagera  wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi  kwa tuhuma ya  kuhusika na ubadhilifu...
 
Watumishi watatu wa manispaa ya Bukoba  mkoani  kagera  wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi  kwa tuhuma ya  kuhusika na ubadhilifu wa fedha za ukarabati  wa shule ya sekondari ya Omumwani inayomilikiwa na jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi CCM Mkoa Kagera

 Hatua hiyo imefutia  agizo la rais  Dr John  Pombe  Magufuli   baada ya kukagua  ukarabati  wa majengo hayo  ambayo  walihamishia wanafunzi waliokuwa wanasoma  shule ya sekondari  Ihungo  na Nyakato kutokana  na tetemeko la ardhi na kubaini  kuwa kiwango cha fedha kilichotumika  ni tofauti na  uhalisia  katika  ukarabati huo.


Katibu tawala mkoa kagera   Diwani Athumani  amewasimamisha  watumishi hao  akiwemo  mhandisi aliyesimamia  ukarabati huo Andondile  Mwakitaru ,pamoja  na mafundi sanifu   Constatine  Felex na  Charles Kafumu baada ya kufanya  ukaguzi  na kubaini kuwa mradi huo ulijengwa chini ya kiwango




Awali  akihojia  na katibu tawala   Diwani Athumani ,mhandisi   Andondile Mwakitaru  amesema   ukarabati  huo umegharimu  shilingi  milioni  19  huku fedha ambazo zilitengwa  ni milioni  23.



Hata hivyo Diwani  Athumani  amemwagiza  kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba  Bw Chibhunu Rukiko kuteua wasimamizi wengine katika mradi huo  wakati  watuhumiwa wakisubiri  kufanyika kwa uchunguzi




About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top