Afisa uhusiano wa TAKUKURU Musa Misalaba amesema, ni kweli wanawashikilia viongozi wa TFF kwa ajili ya mahojiano ambapo wamekuwa wakifanya uchunguzi kwa muda mrefu kabla ya kuamua kuwashikilia kwa ajili ya mahojiano.
“Ni kweli kwamba tunaendelea na uchunguzi dhidi ya viongozi mbalimbali wa TFF na uchunguzi huo tumekuwa nao kwa muda mrefu lakini kuhusu kuwashikilia kwa nini, bado ni siri yetu upande wa uchunguzi, katika uchunguzi tunaongozwa na misingi ya sheria, kanuni na taratibu hatuwezi tukaweka wazi kila jambo.”
“Jambo la msingi ambalo wananchi wanatakiwa kuelewa ni kwamba, tuna uchunguzi ambao tunaendelea nao ambao tumekuwa tukiufanya kwa muda mrefu.”
“Tunaowashikilia bado tuko nao chini ya ulinzi weyu , tunaongozwa na sheria tukapopata tunachokitaka tutawaachia bila kuchelewa. Ushahidi ndio utakaoamua lakini ni lini ni swala kiuchiunguzi, lakini ni siri ya uchunguzi.”
vyombo vya Habari lilimshuhudia Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa akiwa kwenye ofisi za TAKUKURU. Baadae kidogo alionekana pia Makamu mwenyekiti wa Simba Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF akiwasili kwenye ofisi hizo lakini hadi sasa bado hakuna taarifa za ukahika kwamba na yeye (Kaburu) ni miongoni mwa viongozi wa TFF ambao wanahojiwa na taaisi hiyo.
Post a Comment