Serikali wilayani Muleba imetakiwa kutoa elimu kwa
wakulima wa kahawa kuhusu tozo zilizoondolewa na serikali kwa mwaka wa fedha
2017 /2018 ili kuondoa mkanganyiko unajitokeza kwa sasa.
Wito huo umetolewa na wakulima wa chama cha msingi cha Magata wakati wa mjadala maalumu wa kujadili faida wanazozipata wakulima tangu
kuondolewa kwa baadhi ya tozo katika zao
la kahawa .
Miongoni mwa wakulima hao Shabani Huseni na Shabaha Lisa
wamesema kuwa wanasikia taarifa mbalimbali za kuondolewa kodi mbalimbali katika
zao la kahawa lakini hawana elimu ya kutosha kuhusu kodi zilizoondolewa.
Kwa upande wake mratibu wa mtandao wa wakulima Mkoani Kagera MVIWATA Projestus Ishekanyoro amewahimiza wakulima kuwa na desturi ya
kufuatilia masuala yanayoendelea nchini .
Amebainisha kuwa wao kama
mtandao wa wakulima watalifikisha katika sehemu husika ili waweze kulitolea
ufafanuzi.
Post a Comment