Hatimaye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) imemtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa kinyang’anyiro cha urais baada ya kujikingia kura 7,483, 895 sawa na asilimia 98 katika uchaguzi wa marudio uliosusiwa na mpinzani wake mkuu, Raila Odinga.
Kwa
matokeo hayo, Rais Kenyatta na makamu wake William Ruto walikabidhiwa
vyeti vya ushindi na sasa Uhuru anasubiri kuapishwa kuiongoza nchi kwa
miaka mitano ikiwa matokeo hayo hayatapingwa na kufutwa.
Mwenyekiti
wa IEBC, Wafula Chebukati alitangaza matokeo hayo bila kura kutoka
majimbo 25 ya eneo la Nyanza ambalo wafuasi wa Odinga walifanya vurugu
na kusababisha uchaguzi kuahirishwa.
Chebukati
alisema mazingira yaliyokuwa yameandaliwa kwa ajili ya uchaguzi wa
marudio yaliwezesha kuwa wa kuaminika, huru na wa haki.
Akizungumza
mapema, Makamu mwenyekiti wa IEBC Consolata Nkatha alisema kura za
maeneo ambayo hayakufanya uchaguzi hayawezi kuathiri matokeo ya mwisho.
Nkatha
alisema mchakato ulikamilika katika majimbo 266 ambako uchaguzi
ulifanyika na kwamba tume, kwa kuzingatia kifungu cha 55(B)(3) cha
Sheria ya Uchaguzi ambacho kilielekeza marudio kufanyika na hivyo
kusafisha njia kwa rais mteule kutangazwa.
Alhamisi
iliyopita, ulifanyika uchaguzi mpya wa marudio kama ilivyoamuliwa na
Mahakama ya Juu katika uamuzi wa jumla Septemba Mosi uliobatilisha
ushindi wa Rais Kenyatta wa Agosti 8 kwa madai ya kuwepo kasoro na
dosari zilizofanywa na IEBC.
Odinga
alisusia uchaguzi wa marudio akitaka, pamoja na mambo mengine wafukuzwe
maofisa wa tume na mchapishaji wa makaratasi ya kura na msambazaji wa
vifaa vya kiteknolojia.
Hata hivyo, ilikuwa vigumu kuandaa uchaguzi katika majimbo 25 Kisumu, Siaya, Homa Bay na Migori ambako Odinga anaungwa mkono.
Katika
majimbo mengi, uhuni ulikithiri kiasi cha kuzuia kabisa upigaji kura wa
marudio kwani walifunga mageti na kuchomelea kwa nondo na wengine
walizusha ghasia kiasi kwamba IEBC ilishindwa kuwalinda maofisa wake.
Chebukati
alisema Ijumaa iliyopita kwamba maofisa wa uchaguzi walitishwa,
walitekwa au kuteswa na akasema ilitilia maanani sana kokote ambako
maofisa wake walikabiliwa na vitisho.
Uchaguzi
ulifanyika katika majimbo 265 kati ya 290 ya Kenya yakiwemo ya nje ya
nchi ambapo Wakenya waishio Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika
walipiga kura.
Katika
majimbo 266 Rais Kenyatta alipata kura 7,483, 895 yaani kura 719,395
chini yakura 8,203, 290 alizopata katika uchaguzi uliofutwa.
Kwa
kura 7,616, 21 halali zilizopigwa katika majimbo 266 yaliyoshiriki
uchaguzi, idadi hiyo ni sawa na asilimia 42.36 wakati ikipigiwa hesabu
kwa watu 19, 611, 423 waliojiandikisha walioshiriki uchaguzi wa Alhamisi
walikuwa asilimia 38.84.
Uchaguzi
wa Agosti 8 waliojitokeza walikuwa asilimia 79.17 idadui ambayo ilikuwa
pungufu ikilinganishwa na mwaka 2013 waliposhiriki asilimia 86 ambao
Kenyatta alimshinda Odinga katika kinyang’anyiro kikali. Odinga alipinga
matokeo lakini alishindwa Mahakama ya Juu.
Post a Comment