Wadau wa
maendeleo katika Kata
ya Kituntu wilayani Karagwe wamekutana na
kujadiliana juu ya kutatua
Changamoto ya madawati katika shule za msingi kwa kata hiyo.
Hatua hiyo
imefikiwa baada kubaini
upungufu wa zaidi wa madawati 687
katika kata hiyo kwa shule za msingi, hali ambayo imewalazimu viongozi wa
kata kuitisha wadau wa maendeleo ya upatikanaji
wa miti ya kupasua kupata mbao za
kutengenezea madawati ili kunusuru tatizo hilo.
Kwenye kikao hicho Afisa
Elimu wa kata ya kituntu Sabino Gaudini amesema upungufu wa madawati hayo,
umesababaisha watoto kuendelea kukaa chini na wengine kulazimika kubanana
kwenye madawati hayo hali ambayo inaweza kusababisha ufahuru mdogo kwa
wanafunzi hao.
Kuitishwa kikao cha wadau
hao ni kutaka kusaidia kupunguza michango mikubwa kutoka kwa wananchi wa
kawaida ,ambapo mbao zaidi ya 1,300 za awali
zinahitajika kutengeneza madawati 250.
Wamesema kuwa kikao cha
Kwanza kilichoitishwa kiliwashilikisha wadau kutoka kwenye makanisa, Taasisi za
shule na watu binafsi walioweza kuchangia miti 49 na ikiunganishwa na kikao cha
leo miti 61 imepatikana tiyari kwa ajili ya upasuaji wa mbao hizo.
Aidha zimetajwa shule ambazo
zinaitaji madawati hayo kwa sasa ni Shule ya msingi Kinyinya,Katwe,Maboresho,Katembe
ambazo kwa ujumla zimo ndani kata hiyo.
Hata hivyo uongozi wa kata
umeomba wanachi kuwa na mwitikio mzuri katika uchangiaji wa madawati ili
kutatua swala hilo ambalo litasaidia watoto wao kushiliki vizuri masomo yao kwa
ajili ya ufahuru wa masomo yao.
Post a Comment