Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: SUKARI YA BEI ELEKEZI INAPATIKANA HAPA USIWAZE WAPI
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Kutokana na sukari kupanda na kila mmoja kujipangia bei yake manispaa ya bukoba imeteua mawakala wa maduka 42  ya  kuuza sukari kwa wana...

Kutokana na sukari kupanda na kila mmoja kujipangia bei yake manispaa ya bukoba imeteua mawakala wa maduka 42  ya  kuuza sukari kwa wananchi kwa bei elekezi ya serikali ya shilingi 1800 .

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkuu wa wilaya ya BUKOBA JAKSONI MSOME amesema mpaka sasa zimeundwa kamati ndogo ya watendaji ambayo imepangiwa majukumu ili kuhakikisha zoezi linaenda vizuri.

Ametaja majukumu ya kamati hiyo kuwa ni kubaini kiasi cha sukari kinacholetwa kutoka kiwandani kwenda kwa wakala,kutoa mgao wa sukari kwa tasisi maalumu zenye huitaji kama vile mashule hosipital na vituo vya watoto yatima pamoja na kufuatilia maeneo ya kata kama bei elekezi ikizingatiwa.

Amebainisha kuwa viongozi na maafisa watendaji ngazi zote wanajukumu la kusimamia na  kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kwa bei elekezi ya sukari.

Hata hivyo msome amesema kwa mfanyabiashara ambaye atakiuka maagizo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Zoezi hili la kupanga maduka ya kuuzia sukari elekezi limekuja baada ya wafanyabiashara kujipangia bei tofauti na kila mmoja kuuza bei yake kwa kigezo cha sukari kupanda ikiwa kg moja ilikuwa ikiuzwa shilingi 2200 hadi 2300.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top