Uongozi wa Kampuni ya STAMIGOLD ukiongozwa na Meneja Mkuu Mhandisi Denice
Sebugwao walifika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera tarehe 3 Mei, 2016 kujitambulisha na
kumsalimia Mkuu wa Mkoa wa Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu.
Uongozi huo wa Kampuni ya
STAMIGOLD ukiongea na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu walimpongeza kwa
kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mkuu wa mkoa wa
Kagera na kumweleza shughuli wanazozifanya katika Kampuni yao iliyopo Wilayani
Biharamulo.
Mhandisi Sebugwao alimweleza
Mhe. Kijuu kuwa Kampuni ya STAMIGOLD iliuchukua mgodi uliokuwa ukijulikana kama
TULAWAKA mara baada ya kumaliza uchimbaji na Serikali kuuchukua mgodi huo na
kuunda Kampuni ya STAMIGOLD na kuendelea
na uchimbaji kwa mkataba wa miaka miwili kuanzia mwaka 2014.
Mhandisi Sebugwao amesema
kuwa tangu waanze uzalishaji tayari wamejipatia Dollar za Kimarekani milioni 37
aidha, Kampuni hiyo tayari imefanya utaratibu wa kuongeza muda kutoka miaka
miwili hadi miaka 10 ili kuendelea na uzalishaji zaidi.
Mhe. Kijuu alimuuliza
Mhandisi Sebugwao kuhusu mahusiano na huduma wanazozitoa kwa jamii mara baada
ya kuanza uzalishaji. Mhandisi Sebugwao
alisema wanaisaidia jamii inayowazunguka kwa kujenga barabara, zahati, na
vyumba vya madarasa aidha, kutoa huduma
za maji kwa wananchi katika Wilaya ya Biharamulo.
Aidha, matatizo yanayoikumba
Kampuni hiyo STAMIGOLD ni kutumia umeme wa jenereta badala ya umeme wa gridi ya
taifa, wananchi kuvamia mgodi na kuiba mali, Uharibifu wa misitu kuzunguka
mgodi, na wafugaji kuachia mifugo yao katika eneo la mgodi wakati uzalishaji
ukiendelea.
Baada ya maelezo hayo Mhe.
Kijuu aliupongeza uongozi huo kwanza kwa
kuchimba dhahabu wakiwa kama Kampuni ya Wazalendo wa Kitanzania. Pili aliwataka kuhakikisha
wanashirikiana na kikosi cha Jeshi la Wananchi
kilichoko Biharamulo na Jeshi la Polisi kudumisha ulinzi wa mgadi huo.
Pia Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu
aliushukuru uongozi huo kwa kulipa kodi ambapo hadi Mwezi Machi Kampuni hiyo
ilikuwa ilipa Seriaklini bilioni 16 na inategemea kulipa bilioni 8 kukamilisha
bilioni 24. Kuhusu matatizo waliomweleza alisema atayashughulikia na alihaidi
kuutembela mgodi huo ili kujionea uzalishaji wa dhahabu.
Post a Comment